LIGI Kuu Bara bado moto wake hauzimwi kwa sasa ikiwa ni mzunguko wa pili na kwa baadhi ya timu zikimalizia viporo vyao.
Hii hapa ratiba ya wiki hii na mechi hizi zitarushwa na Azam TV, usisahau kulipia king'amuzi chako upate uhondo namna:-
Jumanne Februari 19
Jumanne itakuwa ni mchezo kati ya Mwadui FC dhidi ya Biashara United saa 8:00 Mchana Uwanja Mwadui Complex.
African Lyon dhidi ya Simba Uwanja wa Amri Abeid, Arusha saa 10:00 Jioni.
Coastal Union dhidi ya Azam FC Uwanja wa Mkwakwani Tanga majira ya 10:00 Jioni.
Jumatano Februari 20
Mbao FC dhidi ya Yanga Uwanja wa CCM Kirumba saa 10:00 Jioni.
Mbeya City dhidi ya Tanzania Prisons Uwanja wa Sokoine, saa 10:00 jioni.
Stand United dhidi ya Lipuli uwanja wa Kambarage
Ijumaa Februari 22
Azam FC dhidi ya Simba Uwanja wa Taifa saa 10:00 Jioni.
!!!!Azam wanacheza mara ngapi wiki hii?
ReplyDeleteHii obsessesion na ratiba imekuwa ugonjwa kwenye blog hii
Tena Azam wanasafiri kwa basi wakati Simba wamepanda ndege!!!.
Blog ya kipuuzi...wana obsession na ratiba na matokeo ya Simba!Yani akili kama za kizahera vile!
ReplyDeleteWamebadili headline. Afadhali imekuwa karaha sasa .
ReplyDeleteMbona unaongelea Azam ambaye anacheza jumanne dar wa salaam, unamsahau Simba anaywcheza jumamne Arusha na wanatakiwa wakutane ijumaa?
ReplyDeleteAzam anacheza Tanga jumanne .
ReplyDeleteTatizo la mashabiki wasiojitambua kwa hiyo hapo umeonaje? Walaumu TPLB.
ReplyDeleteBinafsi sioni mantiki ya wale wanaolaumu! Sijajua wanatakaje. Kwa maana hizo timu zote zinazokutana Ijumaa, zote zinacheza jumanne hii ya leo. Cha ajabu ni kipi hapo?!
ReplyDeleteSuala la kupanda Ndege au Kusafiri kwa Basi ni maamuzi ya Uongozi wa timu. Hakuna mpango uliowekwa kwamba ni lazima Simba isafiri kwa Ndege, na ni Marufuku Azam kusafiri na Ndege. Lawama zingine za mashabiki hazina mashiko wala mlengo chanya kwa timu yoyote.