Mchezo namba 270 wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara uliozikutanisha Young Africans na Simba uliochezwa Jumamosi Februari 16,2019 kwenye Uwanja wa Taifa umeingiza jumla ya shilingi Milioni 342,825,000
Mchezo huo uliingiza jumla ya watazamaji 41,266.
VIP A waliingia Watazamaji 546 kwa kiingilio cha Shilingi 30,000 na kupatikana jumla ya shilingi 16,380,000,VIP B na C waliingia Watazamaji 3,185 kwa kiingilio cha shilingi 20,000 ikapatikana jumla ya shilingi 63,700,000,Majukwaa ya rangi ya Machungwa,Bluu na Kijani waliingia Watazamaji 37,535 kwa kiingilio ncha shilingi 7,000 imepatikana jumla ya shilingi 262,745,000
Mgawanyo wa mapato
VAT 52,295,338.98
Selcom 15,170,006.25
TFF 13,767,982.74
Uwanja 41,303,948.22
Young Africans 165,215,792.86
Gharama za mchezo 19,275,175.83
TPLB 24,782,368.93
BMT 2,753,596.55
DRFA 8,260,789.64
SI HABA KWETU YANGA MILIONI 165 ALHAMDULILAH TUNGECHANGISHANA MIEZI MINGAPI KUZIPATA HIZO HAPO NDEGE VIJANA WAMEPANDA KWENDA MWANZA NA WATARUDI DAR NA NDEGE NA TUTASHINDA MECHI YETU NA MBAO MORALI IPO VIZURI
ReplyDeleteWizi mtupu na ujanja ndani hii ndio maana soka la bongo linadidimia siku hadi siku
ReplyDeletehaya mambo wanajitakia vilabu wenyewe kwani hili swala limelalamikiwa muda mrefu BMT ni chombo cha serikali wanaopaswa kuhudumia ni serikali kama vat imelipwa kwanini BMT naye achukue mapato, bodi ya ligi inachukua milioni 24 kwa kazi gani wanafanya wakati hata ratiba kupanga inawashinda, drfa nao wanachukua milioni 8 kwa lipi
ReplyDeleteDuh Kweli Wizi Mtupu Makato Yamezidi So Nataka Kuuliza Wadau Wa Blog Hi Mapato Yanayo Patikana Timu Ngeni Haipati Chochote?
ReplyDeleteTimu ngeni haipati chochote. Simba ilichukua mapato yote mechi ya kwanza.
ReplyDeleteMechi ya kwanza iliingiza milioni 400 na Simba walipata milioni 194.
ReplyDeletewavuja jasho na wakivulini nguvu moja
ReplyDeleteehe eti hell za Kodi za wananchi zimejenga uwanja was taifa,hata aibu hamna timu zinakamuliwa haswa, ndiyo maana panaitwa kwa mchina
ReplyDelete