February 27, 2019


MABINGWA watetezi wa Ligi Kuu Bara, Simba, wameendelea na kasi yao ya ushindi baada ya jana kuwafunga Lipuli FC ya mkoani Iringa mabao 3-1.

Huo ni ushindi wa tano mfululizo wa ligi walioupata Simba tangu waanze kucheza mechi zao za viporo. Ilianza kwa kuifunga Mwadui mabao 3-0, ikaichapa Yanga bao 1-0, African Lyon ikafungwa 3-0, Azam FC nayo ikaambulia kichapo cha mabao 3-0, kabla ya jana Lipuli nayo kufungwa.

Ushindi huo umeifanya Simba kufikisha pointi 48 katika msimamo wa ligi wakibakiwa na mechi sita kuwa michezo sawa na Yanga.

Hii ni mara ya kwanza kwa Simba kuifunga Lipuli kwani kabla ya mchezo wa jana, timu hizo zilikutana mara tatu kwenye ligi na kutoka sare zote.

Katika mchezo huo wa jana uliochezwa kwenye Uwanja wa Samora mkoani Iringa, Simba ndiyo walikuwa wa kwanza kupata bao katika dakika ya tano kupitia kwa Mzambia, Clatous Chama aliyepokea pasi ya Mohammed Hussein ‘Tshabalala’.

Simba baada ya kupata bao hilo, Lipuli waliongeza kasi ya ushambuliaji na kufanikiwa kusawazisha dakika ya 18 kupitia kwa Paul Nonga.

Dakika ya 43, Chama aliifungia Simba bao la pili kwa faulo ya moja kwa moja nje kidogo ya eneo la 18. Timu hizo zilikwenda mapumziko Simba ikiwa mbele kwa mabao 2-1.

Baadaye dakika ya 58, Mnyarwanda, Meddie Kagere aliifungia Simba bao la tatu baada ya kumchambua kipa wa Lipuli, Mohammed Yusuph.

Wakati pambano hilo likiendelea, beki wa Lipuli, Paul Ngalema alipewa kadi nyekundu baada ya kumpiga kiwiko, John Bocco.

Bao alilofunga Kagere jana lilimfanya afikishe 12 sawa na Heritier Makambo wa Yanga na Salim Aiyee wa Mwadui, huku Simba ikiwa imefunga jumla ya mabao tisa katika mechi tatu mfululizo.

3 COMMENTS:

  1. Simba wapo vizuri kinachofurahisha sasa kwa wachezaji wa Simba ni ule uwezo wao wa kulazimisha matokeo. Wachezaji wakubwa kutoka timu kubwa lazima wajitofautishe na wachezaji wa kawaida kwa kufanya vitu visivyozoeleka kufanywa na wachezaji wa kawaida. Kwa mfano ukiangalia mechi ya Jana kati ya Simba na lipuli utaona yakwamba Emmanuel Okwi aligeuka kuwa Cletus Chama na Chama aligeuka kuwa Emmanuel Okwi kimajukumu uwanjani au unaweza kusema Simba walichezesha viungo washambuliji wawili kwa wakati mmoja. Utaona namna gani Okwi alivyopevuka kimpira hivi sasa unamuona kabisa zile hisia za kwamba lazima yeye afunge goli hana kabisa. Okwi anaipigania Simba ipate point tatu iwe isiwe. Okwi yupo tayari kwa lolote katika kujitoa kuipigania Simba ipate ushindi na ameshakutana na misukosuko mikubwa kwa ajili ya kuipigania Simba uwanjani kama vile kuzimia kwa kufanyiwa faulu mbaya,kuumizwa mara kwa mara na mabeki na hata jana alionekana kucheza uwanjani akiwa na bendeji usoni. Hakika Okwi ni miongoni mwa wachezaji wenye kuheshimu majukumu yao ya kazi. Na kwa wachezaji hasa vijana wanaotaka kujifunza juu ya uwajibikaji na nidhamu kwa timu kwa kujitoa kwa ajili ya timu ndani ya mchezo wa mpira basi hawana haja ya kwenda kuangalia mbali labda Mesi au Ronaldo bali Okwi ni darasa tosha . Vyombo vya habari ni taasisi muhimu kabisa duniani hasa katika masuala ya kuelimisha jamii. Na ingekuwa vizuri kwa vyombo vyetu vya habari vya ndani kutumia majina ya watu maarufu na wanaofanya vizuri katika kazi zao hasa katika masuala ya maadili mema ili kutoa mafunzo na uhamasishaji kwa kundi kubwa la vijana hasa wale waliokuwemo kwenye tasnia zinazofanana. Ukimuangalia Okwi kimaadili,je analewa kupindukia sifikirii. Sidhani hata kama anavuta sigara. Je Okwii ni mtukutu uwanjani au muhuni sidhani kama anasifa hizo. Kinachofahamika kwa Okwi kuwa ni mwanafamilia mzuri ana mke na mtoto lakini ukija ukimuangalia kazini kwake utazani hana majukumu mengine isipokuwa majukumu yake ni kuitumikia Simba tu,hii ni nidhamu ya kazi kwa Okwii ni fundisho pia na kuna haja ya kuthamini anachokifanya na kukitangaza bila ya figisu.

    ReplyDelete
  2. This is simba brother,I think watapata majibu mengi sana ya maswali yao, wakati ndio huu.

    ReplyDelete
  3. Umeongea sana alafu mambo ya msingi,ninachokiona ni kutofautiana katka mtazamo maana kwa mtazamo wangu mimi mpaka sasa mchezaji bora kwa simba ningemchagua okwi,ila ndio hivyo mitazamo tofaut lazima atachaguliwa usiyemdhania.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic