KOCHA Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera amesema kuwa suala la nahodha wa Yanga Ibrahim Ajibu kugomewa kupewa mkono na nahodha msataafu, Kelvin Yondani lilizua jambo jipya kwa wachezaji wa Yanga.
Yondani alikuwa nahodha alivuliwa kitambaa na Zahera kitambaa chake akakabidhiwa Ajibu ambaye jumamosi kwenye mchezo dhidi ya Simba alimpa mkono Yondani wakati wa kumtambulisha mgeni rasmi Yondani akaugomea.
Zahera amesema kuwa Yondani alifanya hivyo kutokana na uzoefu wake na alimgomea makusudi na sio bahati mbaya kwani nahodha huwa hasalimii wachezaji wake.
"Tulipokwenda kwenye chumba cha kubadilishia nguo wachezaji wote walimcheka sana Ajibu kwa kusalimia wachezaji wake, Yondani alimwambia kwamba nahodha huwa hasalimi wachezaji wenzake.
"Hivyo taarifa ambazo zinadai kwamba Yondani na Ajibu wana ugomvi sio kweli ni jambo ambalo lilifurahisha timu kwa ujumla kwa sasa tupo Mwanza tukijiandaa kwa ajili ya mchezo wetu dhidi ya Mbao," amesema Zahera.
Haaaaaaaah, Zahera una akili sanaaaaaaa!Yanga tuna shida Zetu lakini Zahera Kuna wakati unatufanya tujione tuko imara sanaaaaaaaaaaa!
ReplyDeleteChaguo sahihi,kwa wakati sahihi!
Tatizo la vyombo vyetu vya habari au baadhi ya waandishi na hata wapenzi wa soka la Tanzania wanakuza sana tukio....hebu tuiache hii tabia ya kulikuza jambo ili kutafuta vyanzo vya habari.....kama hamna habari acheni kuposti matukio ambayo hamna uhakika nayo....hili tukio linakuzwa tu....hakuna bifu lolote lililopo....hebu habari hii iishe tuendelee na mengine
ReplyDelete