February 18, 2019


MABINGWA wa kihistoria wa Ligi Kuu Bara, Yanga wakiwa wamebeba kombe mara 27 bado wana moto baada ya leo kutia timu mkoani Mwanza na kuanza mazoezi kwa ajili ya kujiaandaa na mchezo wao dhidi ya Mbao FC.

Yanga Jumamosi walikuwa Uwanja wa Taifa kumenyana na Simba na walipoteza kwa kufungwa bao 1-0 watacheza na Mbao mchezo wa marudio Jumatano Uwanja wa CCM Kambarage.

Yanga wataingia kwenye mchezo huo wakiwa na kumbukumbu ya ushindi wa mabao 2-0 ambao waliupata kwenye mchezo wao uliochezwa Uwanja wa Taifa.

Yanga itakosa huduma ya kiungo Feisal Salum kutokana na kuwa na kadi tatu za njano alizopata hivyo hatakuwa sehemu ya kikosi kitakachowavaa Mbao FC.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic