Kesi inayowakabiri viongozi watatu wa klabu ya Simba imeendelea leo katika Mahakama ya Kisutu jijini Dar es Salaam huku ushahidi wa pili ukiendelea kutolewa katika kesi ambayo inawakabili waliokuwa viongozi Simba, Evans Aveva, Godfrey Nyange na Zachariah Hans Poppe umeibuka utata.
Utata huo umeibuka kutokana na majina kutofautiana inadaiwa kuwa mnamo Machi, 15, 2016.Evans Aveva na Godfrey Nyange walihamisha fedha kutoka kwenye akaunti ya Simba kwenda katika akaunti ya Evans Aveva ya Barclay's Bank yenye akaunti namba 147002211 na sababu ya kuhamisha fedha ilikuwa ni malipo ya mkopo(loan repayment) toka kwa Simba kiasi cha dola 300,000.
Hata hivyo shahidi wa pili katika kesi hiyo,George Japheth ambaye ni Meneja Biashara wa CRDB tawi la Azikiwe jijini Dar es Salaam aliimbia mahakama katika bank statement imeonyesha fedha zilizohamishwa jina linasoma kama Francis Aveva na wahusika ni waliweza kuandika taarifa hizo wenyewe.
Hakimu Mkazi Mkuu,Thomas Simba amehairisha kesho hiyo mpaka kesho Jumanne ushahidi upande wa serikali utaendelea kutolewa.
0 COMMENTS:
Post a Comment