NA SALEH ALLY
NINAAMINI utakuwa umemsikia Kocha Mwinyi Zahera akiwaelezea waandishi wa habari kwamba amepewa taarifa kuwa kuna timu inanunua wachezaji kwa bei ghali na kadhalika lakini imekuwa ikipita huku na kule kutoa fedha ili Yanga ifungwe.
Zahera ameyasema hayo wakati akizungumza kwenye mkutano wa waandishi wa habari na msisitizo wake ulikuwa kwamba timu hiyo inatoa fedha kwa timu zinazokwenda kucheza na Yanga.
Kwa mujibu wa Zahera, fedha hizo zinatolewa namna hii; kama timu hiyo itaishinda Yanga basi inapewa milioni 10, ikiitoka sare ni Sh milioni 5.
Kocha huyo Mkongoman akaelezea mifano na kutaja Singida United waliyocheza nayo hivi karibuni na JKT Tanzania pia.
Matokeo ya mecho hizo ilikuwa ni sare na ushindi kwa Yanga. Maana yake katika mechi hizo mbili walipata pointi nne.
Huenda haya yanafanyika kama anavyosema Zahera, lakini kwa kocha tena wa klabu kubwa kama Yanga anapaswa kuwa angalau na uthibitisho.
Amesema kuna wachezaji wa zamani wa Yanga walio katika timu hizo wanawaeleza hali namna ilivyo na walivyopewa hizo bakshishi. Basi ni jambo zuri kwa kuusaidia mpira wa Tanzania kama kitu hicho hakitakuwa sahihi.
Sijaelewa kama watakaokuwa wamefanya hivyo wanaweza kukamatwa kisheria, kwa maana walikuwa wakihamasisha timu fulani ishinde. Kuhamasisha maana yake anayetoa kwa ile timu, atakuwa anaiunga mkono.
Ni sawa na yule anayetoa fedha kwa ajili ya kuisaidia timu anayoipenda ili iifunge timu nyingine. Maana yake anatoa morali kwa kikosi.
Naona kuna tatizo kubwa kwa yule ambaye anamhonga mchezaji wa timu husika, mfano atoe fedha kwa mchezaji wa Yanga, afungishe. Huyu anatoa rushwa.
Tunaweza kuangalia na kujadili lakini onyo langu kwa Zahera, aangalie asijihusishe na siasa za mpira wa Tanzania kupindukia. Kama mtaalamu wa mpira anaweza kujikita katika nafasi yake.
Wakati mwingine anaweza kuwa anajazwa maneno na watu wanaomzunguka kumbe nao wanakuwa hawana uhakika. Mwisho msala utamuangukia yeye atakaposhindwa kuthibitisha.
Pia inawezekana akaanza kujichanganya kama mambo anayoyazungumza yatakosa uhakika na taratibu kuanza kumuonyesha ni mtu anayebahatisha na watu wakachukua hiyo na kuipeleka hadi katika kazi yake ya ufundi ambayo mimi ninaamini ni nzuri.
Anachopaswa kukumbuka Zahera ndani ya Yanga kuna watu wasingependa aendelee kubaki kwa kuwa sijawahi kusikia kuna kocha wa Yanga anapendwa na kila mtu.
Kuna wanaozipenda hizi klabu na wale walio kwa ajili ya maslahi yao na hili ninaweza kulithibitisha kupitia yeye Zahera ambaye aliwahi kusema alidanganywa na kuelezwa baadhi ya wachezaji wangesajiliwa, haikuwa hivyo na mwisho wakasajiliwa ambao hakuwataka kwa kuwa tu tayari dirisha lilishafungwa na hakuwa na ujanja.
Tumesikia mara kadhaa wachezaji katika klabu hizi wakilalama kupunjwa maslahi yao au kuzungushwa kwa kuwa walishindwa kugawana fedha na wahusika wanaofanya usajili. Hivyo suala la watu kuwa ndani ya klabu hizi na wakajali maslahi yao zaidi, si geni.
Msisitizo wangu ni kwa Zahera, aangalie asilishwe maneno yasiyo na ushahidi na yeye akageuka tarumbeta la kuyasukuma kwa jamii, mwisho yatamgeukia na wanaomjaza wao wakakaa kimya, watakaa kando wakimuangalia anavyosumbuka.
Zahera ni kocha wa mpira na anaijua kazi yake. Itakuwa vizuri akajikita katika kikosi chake kwa maana ya ufundi kuhakikisha mambo yanakwenda vizuri kwa kuwa tayari ameonyesha mwendo bora.
Zaidi pia itakuwa ni kama suala la hamasa kama ambavyo mara kadhaa amefanya, basi angeendelea kuwapa hamasa vijana wake na kuangalia mipango yake sahihi kuliko kurukia ya wengine kwa maneno ya kupewa, mwisho itamuangusha.
Kweli Saleh Ali umefilisika kimawazo. Uliandika kwa mihemko kwamba madai ya Zahera yachunguzwe na Takukuru.
ReplyDeleteTena kwa msisitizo mkubwa .Siku hata haijaisha unamwonya Zahera kuhusu kulishwa maneno ya uongo!!!!
Mwandishi mzuri ni yule anayefanya utafiti kwenye habari anazochapisha kwani humuongezea merit kwenye uandishi wake.
Saleh umejiangusha sana kujiingiza kwenye madai ambayo hayana ushahidi bali ni hear say.
Leteni ushahidi wa hayo madai ili yachunguzwe kuanza ku back down ni kujishushia heshima na kuwashushia heshima wanaosoma blog yako.
CHUKI dhidi ya timu au unazi wa timu unayoipenda visiharibu uweledi kwenye kazi.
Zahera ni mropokaji nä hapimi anachosema.Timu yake ilipokuwa inashinda hatukusikia haya madai.
Ananikumbusha Mourihno alipokuwa under press kila mtu alimwona adui au dunia yote ipo against him
Naona dalili za ugonjwa huo kwa Zahera.
Kulaumu wachezaji tena kwa majina hakufanywi hadharani na nmakocha wenye weledi kwenye kazi zao.
Kinachonisikitisha ni waandishi wa Tanzania hawamuulizi maswali kuhusu madai yake.Inakuwa monologue na sio dialogue.
Badilikeni.
Kazi Ya Mwandishi Ni Kutupatia Habari.... Katika Hili Simulaumu Saleh Ally Alituandikia Kilicho Toka Kwa Mropokaji Zahera Pamoja Na Kumshauri Zahera Lakini Asiachwe Akahojie Na Takukuru Athibitishe Madai Yaka Au TFF Nayo Sijui Ipo Haijui Kuwa Ligi Ya Tanzania Inachafuliwa Na Wakongo Walio Zoea Vurugu Za Siasa Kwao
ReplyDeleteDanny anacholaumiwa Saleh ni kutoa habari ya upande mmoja. Allegation zinaposemwa basi kama chombo cha habari angewasiliana na vyombo vinavyosimamia mpira.TFF nä bodi ya ligi ili kubaner stori.
ReplyDeleteKudai kuna timu tajiri hakuwezi kusaidia chochote. Ahojiwe watoe details za madai yake nä ushahidi.
Asiachwe hivi hivi.Kwa wenzetu walioendelea madai kama haya yangesabaisha aitwe athibitishe madai yake.
Haya madai yalikuwa smokescreen ya kocha Zahera kwani alijua hawezi kushinda dhidi ya Simba.
ReplyDeleteAlikuwa anawatayarisha wapenzi wa Yanga kisaikolojia.
Madai haya yasinyamaziwe.
Huwezi kuzua tu bila ushahidi. Nashangaa TFF imekaa kimya!!!!
Tuhuma nzito ila yawezekana kabisa mchezo huo wa kununua mechi Yanga wanao siku nyingi hawawezi kukurupuka hafla na kuja na kauli za hovyo kiasi hicho itakuwa sio akili zao zilizowasukuma kumlisha Zahera maneno ya hovyo isipokuwa wamesukumwa na laana ya zambi za nyuma walizokuwa wakitenda. Simba katoka sare na Ndanda,akatoka sare na lipuli fc ya iringa na kama vile haitoshi Simba wakaja kufungwa na mbao fc ya mwanza lakini hatuja wasikia Simba kutoa sababu zisizokuwa nje ya mpira, hatuja wasikia kulalamikia hata hali ya viwanja kuwa vibovu zaidi ya kocha wao kuwahimiza wachezaji wake. Hata Azam vile vile wanapoteza mechi zao na timu za kawaida kabisa ni ushindani wa ligi tu na laiti kama ligi kuu bara ingekuwa na udhamini wa uhakika basi kazi ingekuwepo. Majungu ya Yanga kwa Simba kutokana na mafanikio yao wanayoyapata simba ndani na nje ya uwanja hayata wasaidia kitu yanga .. Yanga wanatakiwa kujifunza kutoka kwa watani wao hao wa jadi ili na wao wakomboke hasa kiuchumi. Yanga wameshachelewa tayari kufuatana na hatua za Simba katika masuala ya kuendeleza club yao, na Yanga wakiendelea kuzubaa basi watateseka sana kwa Simba hata huo upinzani utapotea kitakachobakia ni mtu na kibonde wake .
ReplyDeleteThis comment has been removed by the author.
ReplyDeleteMwandishi nakubaliana nawe asilimia mia moja. Mimi naongezea tu, hivi inaingia kweli akilini Timu kubwa tena Tajiri ikawatumie wachezaji wa timu nyingine ikawape pesa ili waifunge Yanga sh 10m wakiifunga na sh 5m wakitoka sare? Lakini eti taarifa zenyewe zinatolewa na waliokuwa wachezaji wa Yanga ambao sasa wapo kwenye timu hizo, yaani hawaa wachezaji waliotoka Yanga sasa ndio wanaipenda sana Yanga mpaka kutoa taarifa hizo kwa Yanga. Mona kama hiyo ni mbinu za kumlaghai Kocha ili wapewe pesa kwa kisingizio wenzenu wanatupa pesa ili tuwafunge sasa kama hamtaki tuwafunge na nyinyi toeni pesa. Kwa maoni yangu TAKUKURU wamhoji Zahera atoe ushirikiano ili hao wachezaji wote waliotoa maneno hayo wakamatwe watoe ushahidi ili note wanaotuhumiwa kutoa pesa wakamatwe live fundisho. Ni aina ya utapeli huu.
ReplyDeleteReplyDelete
.........Quote..'' ..Majungu ya Yanga kwa Simba kutokana na mafanikio yao wanayoyapata simba ndani na nje ya uwanja hayata wasaidia kitu yanga .. Yanga wanatakiwa kujifunza kutoka kwa watani wao hao wa jadi ili na wao wakomboke hasa kiuchumi. Yanga wameshachelewa tayari kufuatana na hatua za Simba katika masuala ya kuendeleza club yao, na Yanga wakiendelea kuzubaa basi watateseka sana kwa Simba hata huo upinzani utapotea kitakachobakia ni mtu na kibonde wake .''... UMESEMA KWELI UPO SAHIHI MWANDISHI.
ReplyDeleteManeno machache tu; "Mla rushwa hawezi kujitangaza kuwa nimekula rushwa". Sasa hao waliokuwa wachezaji wa Yanga zamani, leo wapo kwenye hizo timu, wanawezaje kujitangaza kuwa tumekula rushwa ili tuwafunge au tutoe sare!. Mawazo mgando ya Zahera hayo sasa.
ReplyDeleteKwa namna moja kubwa sana, mimi binafsi Zahera nilimkubali sana kuwa ni kocha bora na anayejua kazi yake. Lakini kwahaya maneno maneno yake mengi, anazidi kujishusha mwenyewe bila kujua. Naanza kumpunguzia points za ubora. Propaganda za Mpira haziko hivyo anavyoonyesha, atafute namna nyingine ya kumzorotesha mpinzani, sio kwa namna hiyo.