February 26, 2019



KOCHA aliyechukua mikoba ya kocha mkuu mkuu Hans Pluijm na Juma Mwambusi ambao walipigwa chini kutokana na mwenendo mbaya wa kikosi hicho kwenye ligi, Idd Cheche amesema makocha wa kigeni wengi hawatoi ushirikiano.


Cheche amesema kwa muda aliokaa ndani ya Azam FC amepata nafasi ya kuwatambua kwa ukaribu wachezaji kile wanachohitaji hali iliyompa nafasi kupata matokeo chanya kwenye mchezo wake wa kwanza.

"Unajua tatizo la wageni wengi ni kushindwa kutoa ushirikiano kwa wenyeji, wao wakija wanapenda kufanya maamuzi yao ambayo ni sahihi ila uzoefu wangu unanisaidia kupata matokeo.

"Nimekaa na wachezaji nikawajenga kisaikolojia na kuwapa maneno ya nguvu hali ambayo imewafanya wapambane na wapate matokeo chanya," amesema Cheche.

Jana Cheche aliongoza kikosi chake kikashinda mabao 3-0 mbele ya Rhino Rangers na kuifanya itinge hatua ya nane bora.

3 COMMENTS:

  1. Acha ujinga sasa cheche amesaidia nini hapo kwa azam kupata matokeo mazuri?hayo ni matokeo ya mholanzi acha kumpa cheo mtu ambae hana mchango au mchango wake bado sana kwa kipindi chote hiki azam itayumba sana maana lazima atabomoa wakati anatengeneza combinations anayoitaka yeye,subirieni hapa yani matokeo yatakua hovyo na yakusuasua sana kwa kipindi hiki walichomfukuza kocha.

    ReplyDelete
  2. Si mwambusi naya kocha mzawa atakuwa anamsaidia au na yeye hapewi ushirikiano?

    ReplyDelete
  3. UPUUZI MTUPU> CHECHE ALIFUNDISHA AZAM KABLA NA TIMU ILIPOANZA KUYUMBA AKATOLEWA TIMU KUBWA AKAPEWA TIMU YA VIJANA SASA TOFAUTI GANI YA KUJIKWEZA HIVYO? UKIONA MWENZIO KANYOKEWA USIMCHEKE WEWE TIA MAJI UJUE WEWE LAKO LINAKUSUBIRI

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic