February 7, 2019


SIMBA kwa sasa inapitia kipindi kigumu baada ya beki wake Erasto Nyoni kuwa nje ya uwanja sababu ya majeraha, lakini beki huyo anarejea uwanjani kabla hata ya mechi dhidi ya Yanga, Februari 16.

Erasto amekosekana kwa zaidi ya wiki tatu ndani ya kikosi cha Simba tangu alipoumia goti katika michuano ya Mapinduzi mchezo ambao kipindi cha pili ilikuwa ni kero kubwa kwa wachezaji na makocha kutokana na mvua kubwa iliyonyesha ambayo hata hivyo haikumshawishi mwamuzi kuahirisha mchezo huo.

Huo ni mchezo wa tatu mfululizo kwa Yanga kushindwa kupata pointi tatu mkoani baada ya kufungwa na Stand United bao 1-0, kisha ikatoka sare ya bao 1-1 na Coastal na jana suluhu dhidi ya Singida United. Licha ya sare hiyo, lakini bado Yanga inaongoza ligi ikiwa na pointi 55 baada ya kucheza mechi 22.

Imebakiwa na mechi 16 kabla ya kumalizika kwa msimu huu Simba wana pointi 33 katika mechi 14. Yanga itaendelea kusalia mkoani ambapo Jumamosi hii inatarajiwa kucheza dhidi ya JKT Tanzania kwenye Uwanja wa Mkwakwani, Tanga, kisha itarejea jijini Dar es Salaam kwa ajili ya mchezo wao dhidi ya watani wao wa jadi, Simba unaotarajiwa kuchezwa Februari 16, mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa, Dar.

Kocha wa Yanga, Mwinyi Zahera, jana alimuanzisha benchi nahodha wa kikosi hicho, Ibrahim Ajibu ambaye aliingia kipindi cha pili, lakini hata hivyo hakuweza kubadilisha matokeo hayo.

Mbali na Ajibu, pia beki Andrew Vincent ‘Dante’ ambaye alianza mechi iliyopita dhidi ya Coastal Union, jana alianzia benchi baadaye aliingia kuchukua nafasi ya Kelvin Yondani.

Katika rekodi za hivi karibuni, Yondani hakuwahi kufanyiwa mabadiliko kwenye mechi aliyoanza na hii inakuwa ni mara yake ya kwanza.

Wakati Yanga ikitoka suluhu jana, leo Alhamisi Simba itacheza dhidi ya Mwadui kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar.

Simba imepitwa pointi 22 na mechi nane ambazo ni sawa na pointi 24. Kama Simba itashinda mechi zake zote hizo na kuwa sawa kimichezo na Yanga, inamaanisha kwamba itakuwa juu kwa pointi mbili hali ambayo itawarudisha kwenye mbio za kutetea taji lao hilo walilolitwaa msimu uliopita.

Zanzibar mwezi Januari. Beki huyo wakati akiwa nje, Simba imejikuta ikiruhusu mabao 10 kwenye mechi mbili baada ya kufungwa 5-0 na AS Vita kisha tena 5-0 dhidi ya Al Ahly.

Erasto ambaye jana Jumatano aliibuka kwenye mazoezi ya timu hiyo yaliyofanyika Uwanja wa Boko, ameliambia Spoti Xtra kwamba anaendelea vizuri na muda sio mrefu ataungana na wenzake.

“Namshukuru Mungu ninaendelea vizuri nimepata matibabu, Mungu anasaidia ninaendelea vizuri kabisa.

“Nitarejea uwanjani muda siyo mrefu ila kesho (leo) nitaenda kupata vipimo ili nijue lini nitaanza mazoezi, nitarudi uwanjani karibuni tu.

“Ninawashukuru mashabiki wetu kwa kutupa sapoti wasikate tamaa waendelee kuwa na sisi na kitu kikubwa nitarudi uwanjani karibuni,” alisema Erato. Daktari wa Simba, Yassin Gembe kwa upande wake, alisema: “Erasto yuko vizuri na ataanza mazoezi Jumatatu ijayo, mazoezi hayo yatakuwa
mepesi kwa ajili ya kumrudisha uwanjani.

“Kuhusiana na kucheza hiyo itategemea na yeye atakavyoyapokea mazoezi hayo mepesi na juu ya hilo la kipimo ni kweli atapima lakini ni kutaka kujua kwa namna gani tu amepona. “Unajua mchezaji akiumia anapimwa kujua ukubwa wa jeraha lakini pia akipona ni lazima apimwe kuona kwamba kapona kwa kiasi gani.”

1 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic