KIKOSI cha Mashujaa FC kutoka Kigoma kilichoingo'a Simba kwenye hatua ya awali ya kombe la Shirikisho FA, Jana waliambulia joto ya jiwe kwa kuchapwa na Green Warriors mabao 2-1 katika mchezo wa Ligi Daraja la kwanza uliochezwa Uwanja wa Mej.Gen.Isahmuyo.
Green Warriors nao pia waliitoa Simba kwenye hatua za awali kombe la FA mwaka 2017 kwenye mchezo uliochezwa Uwanja wa Chamazi kwa mikwaju ya penalti 4-3 waliwazidi ujanja Mashujaa na kuibuka na pointi tatu.
Kocha Mkuu wa mashujaa FC, Atuga Manyudo amesema kuwa walizidiwa mbinu na wapinzani wao hali iliyowafanya wapoteze kwenye mchezo huo.
"Wachezaji wamepambana kupata matokeo ila haikuwa bahati yetu tulizidiwa mbinu na wenzetu wakaibuka na matokeo hivyo ni muda wetu kujipanga kwa ajili ya michezo yetu inayofuata.
"Mpira ni mchezo wa makosa tulishindwa kutumia nafasi ambazo tulitengeneza wenzentu wakatuadhibu, makosa tutayafanyia kazi na tukuwa na mwenendo mzuri katika mechi zetu za mbele, kikubwa sapoti," amesema Manyundo.
0 COMMENTS:
Post a Comment