February 18, 2019



BAADA ya jana kulazimisha sare ya kufungana mabao 2-2 dhidi ya Singida United,Uwanja wa Samora, kikosi cha Lipuli kimeifuata Stand United mkoani Shinyanga kwa ajili ya mchezo wao wa Ligi Kuu Bara utakaochezwa Uwanja wa Kambarage.

Kocha wa Lipuli, Matola Seleman amesema kikosi chake kinawafuata wapinzani wao kishujaa licha ya kuwa watakuwa ugenini siku ya alhamisi.

"Tumeondoka Iringa kuwafuata wapinzani wetu Stand United, ni timu nzuri na tunaiheshimu ila hamna namna kikubwa tunahitaji pointi tatu, uwezo tunao na nia tunayo tutapambana kupata matokeo," amesema Matola.

Lipuli FC imecheza michezo 26 imejikusanyia jumla ya pointi 36 ikiwa nafasi ya nne kwenye msimamo huku wapinzani wao Stand United wakiwa nafasi 12 baada ya kucheza michezo 27 na pointi zao 30.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic