MWADUI FC leo wanaikaribisha Biashara United kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara, Uwanja wa Mwadui Complex ikiwa ni mzunguko wa 28 wakijivunia mshambuliaji wao Salim Aiyee mwenye mabao 11.
Aiyee kwa sasa amemfikia mbabe wa kutupia, Heritier Makambo wa Yanga ambaye ana mabao 11 akimgaragaza nyota wa Simba, Meddie Kagere mwenye mabao 9 kwenye msimamo wa ufungaji amesema moto wake hauzimi.
"Kikubwa ambacho kinanibeba kwa sasa ni ushirikiano mkubwa ambao naupata ndani ya timu, kila mchezaji anatimiza majukumu yake ipasavyo, nitaendelea kutupia mabao kila ninapopata nafasi," amesema.
Mwadui FC inashika nafasi ya 10 baada ya kucheza michezo 27 kwenye ligi ikwa na pointi 30 huku Biashara United ikiwa nafasi ya 19 pointi 23 baada ya kucheza michezo 25.
Jitahidi sana kuwika na kukalia nafasi za wenyewe kabla mnyama hajatafuna viporo,unadhani mechi saba au nane za simba kagere atashindwa kufunga mabao matatu nakua kinara??acheni kuota mchana jiongezeni
ReplyDelete