February 3, 2019



UONGOZI wa Yanga umesema umejipanga kubeba pointi tatu kwenye mchezo wao wa leo dhidi ya Coastal Union utakaochezwa leo saa 10:00 jioni Uwanja wa Mkwakwani Tanga.

Akizungumza na Saleh Jembe, mratibu wa Yanga, Hafidh Saleh amesema wachezji wana morali kubwa ya kupambana kuokana na aina ya mazoezi waliyoyapata hali inayowapa matumaini ya kuibuka na pointi tatu.

"Ushindani ni mkubwa na kikosi chetu  kipo tayari kwa ajili ya kupambana kwenye mchezo wetu wa leo, tunawaheshimu wapinzani wetu ila matokeo lazima yapatikane.

"Mchezaji wetu ambaye tupo naye Amiss Tambwe ataukosa mchezo kwani bado hajarejea kwenye afya nzuri kutokana na jeraha alilopata kwenye mchezo wetu dhidi ya Biashara United, kikubwa ni pointi mashabiki watupe sapoti," alisema Saleh.

Yanga ni vinara wa ligi kwenye msimamo wakiwa na pointi 53 wamecheza michezo 20 na wamepoteza mchezo mmoja dhidi ya Stand United huku wakishinda michezo 17 na kupata sare michezo miwili 

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic