February 28, 2019


Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe, jana aliliamuru Jeshi la Polisi na Baraza la Sanaa la Taifa (Basata) kumkamata Msanii wa Bongo Fleva, Godfrey Tumaini a.k.a Dudu Baya kutokana na kauli zake.

Waziri Mwakyembe alifikia hatua hiyo baada ya Dudu Baya kumsema vibaya marehemu Ruge Mutahaba. Mara baada ya waziri kutoa amri hiyo, Dudu Baya aliibuka tena na kumwambia waziri asisumbue polisi, wasipeleke magari kumkamata bora wakakamate majambazi, badala yake awaambie polisi atakwenda mwenyewe iwe Kituo cha Polisi Oysterbay, Mabatini, Salender Bridge au Central.

Je, msanii kubishana na waziri kama hivyo ni sawa? Jadili; tafadhali usitukane.

1 COMMENTS:

  1. Acheni uzushi nyie Dudubaya aliomba polisi waelekeze aende kureport kituo gani hakubishana na Waziri...

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic