February 26, 2019

KAMWENE, Lipuli ya Matola imeshindwa kulinda rekodi yake ya kutoruhuhsu kufungwa na kikosi cha Simba tangu ipande ligi msimu wa mwaka 2017/18 baada ya leo Simba kuonyesha ukongwe wake wakiwa Uwanja wa ugenini.

Mchezo wa leo ulikuwa na kasi ya ajabu ambapo iliwalazimu Simba kusubiri mpaka dakika ya tano kuandika bao la kwanza kupitia kwa Clatous Chama baada ya Ally Soso kucheza faulo eneo karibu na eneo la hatari ikapigwa na Emanuel Okwi pembeni kumfuata Mohamed Hussen aliyempa pasi Chama akaandika bao la kwanza.

Wana Paluhengo walionyesha namna walivyo wagumu baada ya dakika ya 18 kufanya shambulizi kali kwa Nonga aliyempa pasi Daruesh Saliboko akarudisha tena kwa Paul Nonga na kuwaacha mabeki wa Simba wakiwa wamenyoosha mikono juu mwendo wa mateka wanashtuka mpira upo kwenye wavu wa Manula.

Simba wakawa wapole kuonyesha wapo pamoja na wanapaluhengo ndipo dakika ya 44 Sonso akacheza rafu nyingine iliyotumiwa vema na Chama kuandika bao la pili, lililodumu mpaka muda wa mapumziko.

Kipindi cha pili timu zote zilikuwa pamoja kwenye kushambulia na kuokoa na ilibidi Simba wasubiri kupeleka salamu nyingine dakika ya 57 Okwi alipotoa pande la pasi na kumfikia Kagere aliyeunyanyua mpira ukazama nyavuni.

Wanapaluhengo walipata pigo dakika ya 67 baada ya Paul Ngalema kuonyeshwa kadi nyekundu na mwamuzi baada ya kumchezea rafu John Bocco, licha ya kuwa pungufu hawakuruhusu kufungwa bao lingine.

Simba wanafikisha pointi 48 wakiwa wamecheza michezo 19 kwa sasa ikiwa ni nyuma ya Yanga wenye pointi 61 wakiwa nafasi ya kwanza huku nafasi ya pili ikiwa kwa Azam FC wenye pointi 50.

3 COMMENTS:

  1. Matora Alisema Atatumia Mbinu Ya Zahara Wa Yanga Kajikuta Anatumia Ya Puljim Wa Azam Fc Aliye Kula 3 Kwa 1 Haahaaa Chama Okwi Kagere Mmemuumbua Matora

    ReplyDelete
  2. Hongereni sana simba kwa kweli mpo vizuri keep it up please. Nilijua kama lipuli watalazimisha kutaka kuifunga Simba basi lazima wafikwe na majanga na si kushangaa kwa mchezaji wao kupata kadi nyekundu. Lipuli kwa hii Simba ya sasa sio sizi yake.

    ReplyDelete
  3. Mwandishi Tunataka Tusikie Tena Matola Anasemaje Baada Ya Timu Yake Kufungwa? Maana Alijinadi Sana Kuahidi Kutufunga Simba Mtafute Matola Umhoji Uteletee Makala Hapa.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic