February 4, 2019


BAADA ya kupoteza mchezo wao wa pili kwa kufungwa mabao 5-0 na Ah Ahly ikiwa ni hatua ya makundi Ligi ya Mabingwa Afrika, kocha wa Simba, Patrick Aussems amesema bado wanamatumaini kusonga mbele kwenye michuano ya kimataifa.

Aussems amesema amejifunza kupitia makosa na amegundua alipokosea atatumia makosa hayo kuwa funzo kwenye michezo yao inayofuata.

"Tumerejea nyumbani salama baada ya kupoteza mchezo wetu ila hilo halitupi taabu kwa sasabu tunajua tulipokosea na tumejifunza kupitia makosa tuliyofanya, tumecheza na timu bora hilo lipo wazi.

"Kuhusu kupoteza bado mashindano yanaendelea hatujatolewa kwenye michuano nafasi yetu ya kufanya vizuri ni kubwa kwa michezo inayofuata, kikubwa ni kufanyia kazi makosa," alisema Aussems.

Simba wanashika nafasi ya tatu baada ya kucheza michezo mitatu ya kimataifa wameshinda mmoja na kupoteza michezo miwili ya hatua ya makundi mchezo wao unaofuata watacheza na Al Ahly Uwanja wa Taifa Februari 12.

1 COMMENTS:

  1. Ausems is jut talk the walk but there is no sign yet that he can walk to talk too much lalala with no change of the game in his team. He need to raise up the fighting spirit from his players otherwise nothing can be achieved on his work . Simba ni kusubiri maumivu mengine makali kwenye ardhi ya Tanzania kutoka kwa Ahly na As vita subir na tuone .

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic