March 15, 2019


MSHAMBULIAJI wa Mwadui FC, Salim Aiyee anazidi kuongeza akaunti yake ya mabao baada ya leo kupachika bao jingine na kumfanya azidi kuvimbisha idadi ya mabao kwenye michezo ya Ligi kuu Bara.

Licha ya timu yake kushindwa kufurukuta mbele ya Stand United kwa kuchapwa mabao 2-1 wakiwa Uwanja wao wa nyumbani, Mwadui Complex.

Stand United wamepachika mabao kupitia kwa Datius Peter na Jacob Masawe.

Bao hilo la leo linamfanya Aiyee kufikisha jumla ya mabao 16 akiwaacha washambuliaji wa Yanga na Simba, Heritier Makambo na Meddie Kagere wenye mabao 12 mpaka sasa Ligi Kuu Bara.

Pia kikosi cha JKT Tanzania leo kimepoteza mchezo wake mbele ya Tanzania Prisons kwa kufungwa mabao 2-0 mchezo uliochezwa Uwanja wa Sokoine, Mbeya.

Mbao ya Tanzania Prisons yalifungwa na Vedastus Mwihabi na Adam Adam.

2 COMMENTS:

  1. jamani amecheza mechi ngapi labda makambo sio kagere

    ReplyDelete
  2. Kwanza waongo jana goli la penati lilifungwa na beki wao na sio mshambuliaji

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic