SIRI NNE ALIZOTOA ZAHERA SIMBA KWENDA KWA AS VITA HIZI HAPA
UONGOZI wa AS Vita umeshtuka mapema na kutuma timu ya watu sita kuweka mambo sawa baada ya kumaliza mechi yao ya nyumbani na Al Ahly katika Ligi ya Mabingwa Afrika.
Watu hao wametua nchini tangu wikiendi iliyopita wakati Simba wakiwa bado wapo nchini Algeria walipokwenda kucheza na JS Saoura na tayari wameshaanza harakati zao za kuweka mambo sawa, wakiwatumia Wakongo waliopo hapa nchini akiwemo Kocha wa Yanga, Mwinyi Zahera.
Hata hivyo, wakati Wakongo hao wakitua nchini tangu Jumapili, Simba wenyewe walitua juzi wakitokea nchini Algeria Chanzo cha ndani kinasema kuwa, Zahera alikutana na Wacongo hao juzi na kuwapa siri kadhaa za Simba.
Moja, Zahera aliwaeleza Vita kuhusu kasi ya mshambuliaji wa timu hiyo, Emmanuel Okwi kuwa anatakiwa kupewa ulinzi muhimu. Pili, aliwaeleza kuwa mashabiki wa Simba wamekuwa wakiipa nguvu kubwa sana timu hiyo na hivyo wawaeleze wachezaji wao wasipaniki.
Tatu, aliwaambia kuwa Simba ni hatari kwenye Uwanja wa Taifa kwani msimu huu haijafungwa mchezo hata mmoja wa ligi na kimataifa, hivyo wanatakiwa kuwa makini.
Ishu ya nne, aliwaeleza kuhusu safu ya ulinzi ya Simba kuwa siyo bora sana kama wapinzani watakuwa na kasi, lakini akiwaonya kuhusu mipira ya krosi kutoka na uwezo wa juu wa mshambuliaji John Bocco na Meddie Kagere.
Hata hivyo, hivi karibuni, Zahera aliliambia Championi kuwa atawapa ushirikiano wa kutosha Vita ili ahakikishe wanaifunga Simba kwa kuwa ni Wakongo wenzake, hivyo habari hii ya chanzo ni uhakika kabisa.
CHANZO: CHAMPIONI
mtu kwao
ReplyDeletempaka sasa haijafungwa goli hata moja na timu ya nje uwanja wa Taifa kwa mashindano haya na inamfungaji bora wa mashindano
ReplyDeleteAlyosahau kuwaambia ni kuwa safu ya ulinzi imeimarika kwa kuwaongeza zana na nyoni, kasahau kuwaambia kauli mbiu za simba kuwa yes we can na ile ya kila mtu ashinde kwake mahesabu ni mwishoni
ReplyDeleteZahera angekuwa mkweli na muaminifu kwa timu yake yanga asingebakia hapa Dar lakini kabakia hapa kushirikiana na kocha wa vita kuiua timu ya nyumbani na naamini ingekuwa timu imetok kwao Congo kuja kucheza na yanga basi pia angeipa siri timu kutoka nchini kwake namna ya kuifunga yanga. Angeweza kuifuata timu yake huko Iringa kwakuwa muda alioupata hapa wa kukaa na timu ya vita toka ifike ulitosha kuwapa maelekezo ya kuifunga simba na baadae kuondoka na yanga luelekea huko Iringa
ReplyDeleteTujifunze uzalendo ndio kitu nilichojifunza kwa Zahera haitakuwa ajabu Leo kuwaona wapuuz flani wakihanikiza upnande wa vita na baada ya mechi wakienda makwao kuomba ugali wa baba zao wenye mapenz na Simba. #Do or Die
ReplyDeleteUzalendo mgeunza miaka minne mfululizo iliyopita, mmezaja jezi za mitimu pinzani na yanga ili kuzisapoti dhidi ya yanga leo mnaomba sapoti ya yanga pambaneni na hali yenu acheni kulia lia ktk media
DeleteUzalendo mgeunza miaka minne mfululizo iliyopita, mmezaja jezi za mitimu pinzani na yanga ili kuzisapoti dhidi ya yanga leo mnaomba sapoti ya yanga pambaneni na hali yenu acheni kulia lia ktk media
DeleteSemeni yoooooooote mtoe upepo mioyoni mwenu mpone. Simba baadae tunaingia uwanjani na lengo moja tu, tunataka point 3 na kiuhalisia ukiniuliza nithibitishe nitakujibu YES WE CAN!
ReplyDeleteMechi zinazosubiriwa kwa hamu leo;
ReplyDelete1. Simba FC (bingwa wa tz) vs AS Vita (bingwa wa DRC)
2. Lipuli FC(msimu wa pili) vs Young Africans (wakongwe tz)
Kweli wewe umekuwa bogasi kabisa, vita hawamjui Okwi au Kagere au Boko? Umekuwa mjinga sana kila kukicha
ReplyDelete