March 14, 2019


IKIWA zimebaki siku tisa kabla Taifa Stars haijacheza na Uganda kwenye mchezo wa kutafuta tiketi ya kucheza Kombe la Mataifa Afrika kiungo wa Yanga, Ibrahim Ajibu, amemtumia kocha wa timu hiyo ujumbe kwa vitendo.

Mashabiki wa soka wamekuwa wakinung’unika chinichini kutokana na kocha wa Stars, Emmanuel Amunike kutomwita kiungo huyo kwenye timu ya taifa pamoja na kwamba amekuwa akifanya mambo makubwa uwanjani.

Ajibu wikiendi iliyopita alionyesha kuwa bado yupo kwenye chati baada ya kupiga pasi yake ya 15 ya bao kwa msimu huu baada ya kuiongoza timu yake kushinda kwa mabao 2-1 dhidi ya KMC. Huu ni ujumbe tosha kwa kocha huyo kuwa anakosea kutomjumuisha mchezaji huyo kwenye timu hiyo.

Mbali na huyo, pia Amunike ameshindwa kumuita kinara wa ufungaji kwenye ligi kwa sasa Salim Aiyee wa Mwadui ambaye amefunga mabao 15. Aiyee naye alimtumia ujumbe kocha huyo kwa kufunga bao moja wikiendi iliyopita baada ya timu yake kuifunga Mbeya City mabao 3-1.

1 COMMENTS:

  1. Hamna jipya.Hata wengine ambao hawajaitwa ikiwamo mfungaji bora hadI sasa wanamtuma salamu kwa Amunike.habari hii ni ya wishful thinking!Kutamani tu!Ndiyo maana kila habari ya uchaguzi wa Yanga lazima picha ya Manji iwekwe.Hagombei hataki kurudi lakini picha inawekwa tena na tens.Hebu fikiria uchaguzi ulioisha wa TFF, haikutokea lakini ingekuwa akili finyu kuweka picha za Malinzi pale uchaguzi ulipoongelewa.Saleh jembe mnaweza andika taarifa za maana na nzuri!Ulichoandika ni dalili za obsession..Lazima Ajibu aitwe Taifa stars.Move on!Na usifute ujumbe wa wadau!Au futa kabisa habari hii

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic