UONGOZI wa timu ya Alliance, umesema kuwa kwa sasa umewekeza akili kwenye mchezo wao wa kombe la shirikisho dhidi ya Yanga utakaochezwa Machi 30 Uwanja wa CCM kirumba ili kulipa kisasi baada ya kufungwa mchezo wao wa ligi.
Akizungumza na Championi Jumatano, Ofisa Habari wa Alliance, Jackson Mwafulango alisema "Wanajua kwamba wanakuja kucheza na timu ya aina gani, tunawaheshimu wapinzani wetu kutokana na ukongwe wao, ila kwa hili watatusamehe ni lazima tuwanyooshe.
"Ushindani ni mkubwa na kwa kuwa mpira ni dakika tisini basi wachezaji wetu wamepewa mbinu mpya na kali ili kuumaliza mchezo wetu mapema, hesabu zetu ni kuona tunawafunga Yanga kisha tutinge hatua ya fainali na kutwaa kombe hakuna kingine," alisema Mwafulango.
debe shinda haliishi kutika
ReplyDelete