PAUL Bukaba, bao lake la kwanza msimu huu akiwa ndani ya Simba alilofunga dk ya 52 akimalizia pasi ya Said Ndemla limemuibua kocha mkuu Patrick Aussems kuzungumzia uwezo wa mchezaji huyo.
Kagere alikamilisha ushindi baada ya dakika ya 56 kupachika bao kwa mkwaju wa penalti baada ya mchezaji wa Ruvu Shooting kumchezea rafu Adam Salamb ndani ya 18.
Aussems amesema kuwa kiwango cha mchezaji wake Bukaba ni sawa na wachezaji wengine hivyo hashangai kumuona akiwa kwenye ubora wake.
"Jambo la kawaida kwa wachezaji wangu, ninawafundisha wote kuwa kwenye usawa hakuna ambaye ni bora kuliko mwenzake, bado tuna kazi ya kufanya hivyo ni lazima tushirikiane," amesema Aussems.
Ushindi huo unaifanya Simba kufikisha pointi 54 baada ya kucheza michezo 21 kwenye msimamo wakibaki nafasi ya tatu huku vinara wakiendelea kubaki Yanga wenye pointi 67 huku Azam wakiwa nfasi ya pili na pointi 59 wote wamecheza michezo 28.
0 COMMENTS:
Post a Comment