March 20, 2019


Na George Mganga

Wadhamini wakuu wa klabu za Simba na Yanga, Kampuni ya SportPesa, imeahidi kutoa kitita cha shilingi za kitanzania, milioni 50 kwa timu ya Simba.

Fedha zinatolewa zikiwa mahususi kwa ajili ya kuipa hamasa Simba kutokana na kutinga hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi wake hapa nchini, Abbas Tarimba, amesema kutinga kwa Simba katika hatua hiyo kubwa ni jambo la kujivunia kwa Simba na taifa kwa ujumla.

"Kufikia hatua ya kuingia hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika si jambo dogo, unaweza kuona Simba wamejitahidi kwa kadri ya uwezo wao.

"Hii imeweza kutoa heshima si kwa Simba pekee bali taifa kwa ujumla.

"Sisi kama SportPesa tutatoa kiasi cha shilingi za kitanzania milioni 50 kwa Simba kuingia hatua ya robo fainali, Ligi ya Mabingwa Afrika.

"Tunapongeze Simba, wachezaji pamoja wa wanachama wake kwa kuisaidia timu kutinga hatua hii, ni fahari kubwa kwetu kama SportPesa.


"Ni matumaini yetu kwamba kadri Simba inavyofanikiwa basi tunawaomba wanachama na mashabiki wa Simba watupe sapoti nasi kama SportPesa ya kucheza huduma zetu.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic