March 3, 2019


Babu aliyejizolea umarufu mkubwa nchini kupitia dawa ambayo ilisaidia kuponya magonjwa mbalimbali ikiwemo kisukari, Mchungaji Mstaafu wa kanisa la Kilutheri, Ambilikile Mwasapile, ameitabiria klabu ya Simba kutwaa ubingwa wa ligi msimu huu. Imeelezwa.

Taarifa imeeleza kuwa Mwasapile amesema kuwa ameoteshwa na Mwenyezi Mungu juu ya ubingwa wa msimu huu kuwa Simba inaenda kuutetea na hii yote ni kutokana na kikosi ambacho inacho.

Mchungaji huyo mstaafu amesema hata msimu uliopita alisema Simba itachukua ubingwa baada ya kupata maono kutoka kwa MUNGU na hatimaye ikawa hivyo.

Aidha pia katika msimu wa juzi 2016/17 Mwasapile aliitabiria Yanga kuchukua kikombe cha ligi na ndoto hiyo ikafanikiwa vema kwa Yanga na kufikisha taji la 27 kwenye ligi.

"Mungu tayari amenipa maono ya soka kwa mwaka huu timu ya Simba itakuwa bingwa wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara msimu huu",

"Ndiyo maono yangu niliyoyapata. Mwaka jyuzi nilisema Yanga itachukua ubingwa ndiyo ilivyo na mwaka jana nilisema Simba itakuwa bingwa ikawa hivyo na sasa nawaambia wapenda soka wote Simba bingwa msimu huu" alisema.

Wakati huo Simba ambayo ameitabiria itakuwa bingwa inashuka dimbani CCM Kambarage, Shinyanga kucheza dhidi ya Stand United katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Simba inacheza na Stand ukiwa ni mchezo wa raundi ya pili baada ya ule wa kwanza kumalizika kwa Stand kufungwa mabao 3-0 kwenye uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Wekundu wa Msimbazi wanaingia kukipiga na Stand huku wakiwa nafasi ya tat ya msimamo wa ligi wakiwa na alama 48 nyuma ya Yanga walio na Azam FC.

Yanga ndiyo ipo kileleni ikiwa na alama 64 huku Azam walio nafasi ya pili wakijizolea alama 53.

1 COMMENTS:

  1. Usitukumbushe utapeli wa huyu babu tafadhali,kuna watu wana machungu naye kwa kupoteza wapendwa wao kwa utapeli wake halafu na wewe unamleta tena huku

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic