March 3, 2019


KOCHA wa lipuli, Seleman Matola amesema kuwa licha ya kupoteza mbele ya Simba bado anakiamini kikosi chake ni imara kitakwenda kukomba pointi tatu ugenini leo Uwanja wa Kaitaba, Kagera.

Lipuli ambao walipoteza mchezo wao wa kwanza mbele ya Simba baada ya kucheza nao michezo mitatu tangu ipande ligi msimu wa 2017/18 walikuwa wanaishia kugawana pointi moja.

Akizungumza na SpotiXtra, Matola alisema :- "Simba wametuongezea hasira ukizingatia mchezo wetu wa nyuma pia dhidi ya Stand United tulipoteza sasa kinachofuata ni kutafuta pointi tatu mbele ya mpinzani wetu Kagera Sugar.

"Ligi kwa sasa ni ngumu na kila timu inapambana kutafuta ushindi, licha ya ratiba kubana tunapambana na wachezaji nimekaa nao nimerekebisha makosa yao ambayo wamemeyafanya kwenye mechi zetu zote zilizopita,' alisema Matola.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic