GADIEL Michael, mwenye pasi mbili za mabao kwenye ligi ndani ya Yanga, na msumbufu akiwa Uwanjani ameelekea nchini Afrika Kusini kwa ajili ya majaribio kwenye klabu ya Bidvestwits inayoshiriki ligi kuu.
Beki huyo ambaye anaingia kwenye rekodi za mashujaa waliovunja rekodi ya miaka 39 ndani ya timu ya Taifa kwa kupeperusha vema bendera ya Taifa kufuzu Afcon mwaka 2019 mwezi Juni nchini Misri.
Taarifa zimesema kwamba beki huyo atakuwa nchini Afrika Kusini kwa muda wa wiki mbili kwa ajili ya majaribio.
Klabu hiyo inashika nafasi ya pili nchini Afrika Kusini huku vinara wakiwa ni Mamelod Sundowns.








Namtakia mafanikio mema ktk majaribio yake
ReplyDelete