March 20, 2019




Upangaji ratiba wa robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika umekamilika huku mabingwa wa Tanzania, Simba wakipangiwa kuvaana na TP Mazembe kutoka DR Congo.

Simba itaanzia nyumbani kutokana mfumo wa michuano hiyo kwa kuwa walimaliza wakiwa nafasi ya pili katika Kundi D.

Upangaji huo wa ratiba unaendelea jijini Cairo, Misri na Simba imewakilishwa na CEO wake Crescentius Magori na Mwenyekiti wake, Sued Mkwabi.

Simba ilimaliza kundi D katika nafasi ya pili na ikajulikana mapema Kuwa ina nafasi ya kukutana na kati ya timu tatu zilizokuwa vinara wa makundi ambazo ni Waydad Casablanca, TP Mazembe au mabingwa watetezi, Esperance.

Constantine Vs Esperance
Sundowns Vs Al Ahly
Horoya Vs Wydad
Simba Vs TP Mazembe

7 COMMENTS:

  1. Ule usemi kuwa mwenzio akinyolewa wewe tia maji utatimia kwa Tp mazembe . iwapo zahera aliwapa mbinu wakashindwa , sisi mbwana samata mbinu atakazotupa tutazitumia ipasavyo kuwamaliza mazembe

    ReplyDelete
  2. Tuna imani na kikosi chetu, uongozi, benchi la ufundi na mashabiki wetu wote. TP Mazembe mwaka huu wawe waangalifu maana Simba hii ni mpya na malengo yao mapya tukutane kwa Mkapa na Congo DRC hakuna mbui mungu yupo.

    ReplyDelete
  3. Simba iimarishe idara ya ulinzi na ushambuliaji.. Otherwise watafunga machache nyumbani alafu ugenini alafu wanapigwa mengi kupita zile hamsa hamsa!

    ReplyDelete
  4. Hatutakubali kupigwa hamsa tens Nina imani na kiraka Nyoni

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic