March 18, 2019


BAADA ya kikosi cha Azam FC kuwa chini ya kocha Idd Cheche wengi wanapenda kumuita Ole Gunnar amevunja rekodi ya bosi wake Hans Pluijm kwa kufunga mabao mengi mara mbili zaidi ya Mholanzi huyo.

Mpaka sasa Cheche ameongoza Azam kupata ushindi kwenye mechi tatu za ligi na moja ya Shirikisho. Cheche amekusanya jumla ya mabao 16 kwenye michezo minne ambayo ni sawa na wastani wa mabao manne kwenye kila mchezo ambao wanashuka uwanjani kwa sasa wakati Pluijm alikusanya mabao sita kwenye mechi nne za mwanzo.

Cheche alishinda dhidi ya Lyon, Uwanja wa Uhuru kwa mabao 3-1, ikiwa ni mchezo wa ligi na akashinda mchezo wa Shirikisho dhidi ya Rhino Rangers Uwanja wa Azam mabao 3-0, kabla ya kuinyoosha JKT Tanzania mabao 6-1 na juzi kumaliza kwa Singida United kwa ushindi wa mabao 4-0.

Pluijm kwenye michezo yake minne ya awali alikusanya jumla ya mabao sita tu ikiwa ni michezo ya ligi na michezo hiyo ilikuwa dhidi ya Mbeya City 0-2, Ndanda 0-3, Alliance 0-1 na alitoka sare na Lipuli michezo yote Uwanja wa Azam Complex.

Azam ipo nafasi ya pili baada ya kucheza michezo 28 imejkusanyia jumla ya pointi 59 kibindoni kwa sasa.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic