BEKI Kiraka wa timu ya Tanzania Prisons, Salum Kimenya ameonyesha uwezo mkubwa ndani ya kikosi chake kwa kuwapiga bao washambuliaji wa kikosi hicho pamoja na wale wa Simba kutokana na juhudi zake za kufumania nyavu.
Mpaka sasa ndani ya Prisons Kimenya ndiye kinara wa upachikaji mabao ambapo amepachika mabao sita huku anayefuatia ni nahodha wa kikosi hicho Jumanne Elifadhili mwenye mabao matano.
Kwa upande wa Simba mshambuliaji Adam Salamba ana mabao manne huku kinda Rashid Juma akiwa hana bao hata moja kwenye Ligi Kuu msimu huu.
Pia hata ndani ya kikosi cha mabilionea Azam FC, mshambuliaji Donald Ngoma amepigwa chini kwani ana mabao matano mpaka sasa.
Kimenya amesema kuwa hesabu kubwa akiwa ndani ya Uwanja ni kuona namna gani wanabeba pointi tatu suala la kufunga ama kutofunga yeye hata hafikirii.
"Tupo kwenye wakati mgumu kwa sasa kazi yetu ni moja kuona namna gani tunapata pointi tatu kwenye michezo yetu yote ambayo tunacheza hivyo mapambano yanaendelea," amesema Kimenya.
Kinara wa mabao kwa sasa ni Salim Aiyee wa Mwadui FC ambaye ametupia mabao 14 huku Kimenya akifunga mabao sawa na nahodha wa Yanga Ibrahim Ajibu.







Upumbavu mkubwa. Unalinganisha na washambuliaji wa Simba pekee. Kwani Simba pekee ndio ipo kwenye ligi?Hizo timu zingine hazipo. Obsession na Simba imekuwa ugonjwa .
ReplyDeleteThis comment has been removed by a blog administrator.
ReplyDeleteHata ukifuta tutarudia kuandika mnachokifuta...Hivi akili yako ni finyu kiasi gani kutambua kuwa Simba katika ligi ni ya tatu?Inakuwaje sasa huyo beki noma akawapiga bao Simba pekee na sio wanaoongoza ligi?Hebu kuwa mstaarabu na kuacha kuandika habari za kishabiki hapa.Blog yenu inaheshimiwa nyie mnajivua nguo hadharani mtadhani ni wagonjwa wa akili...kwa MTU mwenye akili timamu angeandika hivi eti huyo mchezaji amewapiga bao washambuliaji wa timu zote TPL...Inawezekana kabisa na Ally Saleh nae ni akili sawa na wafanyakazi wa blog yake..Hii blog kuna obsession kuhusu Simba ambayo sasa imefikia kiwango cha afya ya akili!unahitaji tiba ndugu mwandishi...HEBU JARIBU KUKUA hata kidogo tu!
DeleteHuyu mwandishi ni Mcenge wa akili.
ReplyDeleteIngekuwa busara kwa blog inaojihishimu kuwa makini na vitu mnavyoviandika.Huu upuuzi ulioandikwa hapo juu kamwe haukupaswa kuandikwa kwani ni kama personal attack kwa ajili ya wachezaji timu fulani tu midhani ya kazi ipo wapi?
ReplyDeleteMsifute maoni ya wadau!Kama mnapiga keki mbaya ileni wenyewe..Kaeni chini mjiulize na mfanye tathmini hicho kitu mlichoandika ni sawa?Kulikuwa na haja gani ya Kuandika mshambuliaji kinda wa Simba hajapata bao..Kwa magoli anayofunga Yanga ya au 1-0 au 2-1 ni wachezaji wangapi Yanga hawajapata mabao?Mpuuzi kweli?Hivi karibuni mmekuwa na tabia kuandika live match ya za Simba...kwenye kichwa cha habari inaonyesha Simba INA bao tatu...Lakini ndani ya live update hakuna goli linakuwa reported!Acheni ujinga na gere za kitoto!
ReplyDelete