June 16, 2021

 


MSHAMBULIAJI wa DC Motema Pembe ya DR Congo Kadima Kabangu amesema kuwa anawasubiri Simba wamalize michezo ya ligi kuu pamoja na Kombe la Shirikisho la Azam FA, ili aweze kufanya mipango ya kuja nchini kukamilisha mazungumzo ya usajili wake.

Kabangu ameweka wazi kufanya mazungumzo na kocha mkuu wa kikosi cha Simba, Didier Gomes.

 

Akizungumza na Championi Jumatatu, Kabangu alisema kuwa viongozi wa Simba walimwambia kwamba asubiri wamalize mashindano ambayo wanashiriki kwa sasa ikiwa ni pamoja na Kombe la Shirikisho pamoja na ligi ili waweze kufanya mazungumzo ya kukamilisha usajili.

 

“Tayari nimeshaongea na Simba kuhusu ishu ya usajili na kwa sasa nawasubiri tu wao wakamilishe michezo ya ligi pamoja na kombe la FA ili niweze kukamilisha usajili wangu ikiwa ni pamoja na kuja Tanzania.

 

"Simba wao ndiyo wameniambia hivyo, kocha Gomes yeye amenithibitishia kuwa nipo katika mipango yake kwa ajili ya msimu ujao na mimi nipo tayari kujiunga na Simba na kilichobaki nawasubiri tu wao,”alisema mchezaji huyo.

9 COMMENTS:

  1. Waungwana kimya lakiniwalengwa wenyewe ndio wanotangaza kwakuona fahari kubwa kujiunga na timu yenye kuheshimika

    ReplyDelete
  2. Hongera sana Mnyama. Nifahari kwa wana Simba wote. Kimia kimia

    ReplyDelete
    Replies
    1. Jifunze kiswahili dogo.....kimia kimia ndo nini??

      Delete
    2. kwani hujaelewa? Acha kujitoa ufahamu mvaa suruali chini ya makalio,umeona hili tu idiot.nenda kashauri utopolo wajirekebishe na wapunguze mbwembwe zisizo na tija wala ulazima, tayari injinia ameshasajili wakimataifa karibia kumi. Sasa sijui yanga inavunja kikosi. Alafu msimu ukianza mnafungwa tu mpaka ligi inaisha.

      Delete
  3. Duh kila msimu yanga wanajenga kikosi. Sasa lini wataanza kuelewana?

    ReplyDelete
  4. Wakishinda mechi za mwanzoni utasikia mwaka huu makombe yote yetu, wakianza kufungwa utasikia kikosi bado kipya hawajaelewana, mara hoo tatizo kocha, mara hoo simba inabebwa, mwishonni wanaanza kususia mechi.... Wakati wenzao wanaangalia jinsi gani watashinda mechi zao za mwishoni ili wachukue ubingwa wao wako bize na usajili..... Badilikeni nyie

    ReplyDelete
  5. Dah... ni kweli mambo ya simba ni kistaarabu. Nafikiria ni lini na sisi yanga tutabadilika

    ReplyDelete
  6. Simba tunataka wachezaji sio wakujaribu na sio walioshindwa au waliokaa benchi team Fulani Kama tunataka kutinga next season hatua ya nusu Hadi fainali

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic