March 1, 2019



MABINGWA wa kihistoria wa Ligi kuu Bara Yanga ambao wamebeba ubingwa mara 27 kesho watamenyana na Alliance ya Mwanza mchezo wa ligi na watakosa huduma ya wachezaji wao watano.

Wachezaji hao ambao wataukosa mchezo wa kesho ni pamoja na Andrew Vincent anayesumbuliwa na maumivu ya  misuli, Pius Buswita ambaye hakujumishwa ndani ya kikosi.

  Raphael Daud anasumbuliwa na maumivu ya goti, Baruani Yahaya anasumbuliwa pia na maumivu ya goti pamoja na  Juma Mahadhi.

Mchezo wa kesho utakuwa wa 26 kwa vinara hao wa ligi ambao kwa sasa wamejikusanyia kibindoni pointi 61. 

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic