HIVI NDIVYO SIMBA ITAKAVYOINGIA HATUA YA ROBO FAINALI CAF LEO
Ni hesabu tu
Mungu akijaalia tukishinda leo na Al Ahly akatoka sare au kumfunga Vita tutakuwa tumefuzu kwa Robo fainali!
Ikitokea tumedroo au kupoteza bado tunawasubiri Vita Jumamosi ijayo hapa Dar.
Na kwa kuwa Timu zikifungana Points baina yenu, hawaangalii idadi ya magoli kwanza bali head 2 head (matokeo ya jumla ya mechi zenu) ni vema kulinda hiyo head 2 head na Soura, sababu ikitokea akatufunga (kwa bahati mbaya) na kisha akapata sare na Ahly wiki ijayo kisha na sisi tukamfunga Vita, sote tutakuwa na Points tisa, na hapo ndiyo head 2head inapokuja!
Nadhani tuna nafasi kubwa bado, muhimu leo tumalize kazi.
Na Haji Manara (Ofisa Habari wa Simba)








0 COMMENTS:
Post a Comment