MANJI AKUTANA NA KOCHA YANGA
KOCHA wa Yanga, Mwinyi Zahera amewahakikishia mashabiki wa Yanga kwamba amezungumza na Yusuf Manji uso kwa uso kwa mara nne na uwezekano wa kurejea Jangwani ni mkubwa.
Zahera ambaye ni Kocha wa Yanga mwenye uraia wa DR Congo na Ufaransa, amekiri kwamba Mwenyekiti huyo wa zamani wa Yanga ni miongoni mwa viongozi wachache wenye akili sana na anajua mambo.
Kocha huyo mwenye Diploma ya Ukocha ya Uefa aliyoipata Ufaransa, amesema wakati akipiga stori na Manji alikuwa na Viongozi wengine wa Yanga Jijini Dar es Salaam hivik aribuni. “Nimezungumza na Manji kama mara nne tofauti, tumekutana kwenye vikao tofauti nikiwa pamoja na viongozi wengine wa Yanga.
“Tumezungumza mambo mengi sana kuhusiana na Yanga na amezungumza na sisi kwa uwazi kabisa, ila nlichokiona anasubiri kwanza hali ikae sawa,”alisema Zahera alipofanya ziara juzi Jumanne kwenye ofisi za Spoti Xtra zilizopo Sinza Mori Jijini Dar es Salaam.
“Inaonekana kuna sehemu ndani ya Yanga kuna baadhi ya vitu ambavyo vinakwenda kwenye hali fulani ambayo haimpendezi sana ndiyo maana hajaweka fedha yake kwenye uendeshaji. Maana unajua yule ni mfanyabiashara hawezi kuweka fedha tu bila kuwa na mamlaka nazo.
“Unajua mimi nikikaa na wewe dakika tano naweza kujua una akili au huna. Ila baada ya kikao cha Manji niliwaambia wale viongozi kwamba huyu jamaa anajua, ana akili sana.
“Ukimsikiliza mipangilio yake na kile anachokisema ni ukweli kabisa na ni vitu ambavyo vinatekelezekana na vinaweza kuifanya Yanga ikapiga hatua. “Kwa jinsi nilivyomsikiliza na kumuelewa Manji atarudi Yanga, atarudi tu ni suala la muda tu,” alisema Zahera na kusisitiza kwamba Manji anaona huruma sana mambo yanavyokwenda sasa ndani ya Yanga.
CHANZO: SPOTI XTRA
Hadithi hizo tumeshazisikia zaidi ya mara mia na hayo ni majaribio ya kuwazuwia wale wachezaji wanaoamuwa kuihama timu hiyo na wakishafanikiwa Manji hatoonekana na bakuli ndilo litalochukuwa pahali pa Manji
ReplyDeleteInaonekana kuna sehemu ndani ya Yanga kuna baadhi ya vitu ambavyo vinakwenda kwenye hali fulani ambayo haimpendezi sana ndiyo maana hajaweka fedha yake kwenye uendeshaji. Maana unajua yule ni mfanyabiashara hawezi kuweka fedha tu bila kuwa na mamlaka nazo.
ReplyDeleteUKIISOMA HIYO AYA KWA UMAKINI KIDOGO TU ANAWEZA KUJUA KWAMBA KUNA NINI AMBACHO KINAENDELEA NDANI YA KLABU AU KUNA PICHA GANI KWA SABABU HUWEZI KUJENGA NYUMBA MOJA NA MTU AMBAYE AMUAMINIANI AU KATIKA SERA ZENU HAZIENDANI KWA MAANA HIYO HAPO HAKUTAKUWA NA MAELEWANO NA HATA KAMA KUTAKUWA NA MIJADALA LAZMA IWE YA KUARIBIANA NA SIO YA KUJENGA KWA SABABU MMOJA KATI YA MDHAMINI NA WANACHAMA AU WAJUMBE AMA VIONGOZI HAWAMTAKI KWA HIYO TUENDELEE NA TAMTHILIA YA YANGA VS MANJI...........