March 2, 2019



LIGI Kuu Tanzania Bara kwa sasa inazidi kukata mbunga huku ushindani ukizidi kuonekana siku hadi siku kwani hakuna timu ambayo inakubali kuonewa.

Licha ya kukosekana kwa mdhamini mkuu wa ligi hali inayofanya mwendelezo wake kwa baadhi ya timu ambazo hazina mdhamini kwenda kwa kusuasua ila burudani bado inaonekana.

Mpaka sasa kuna wachezaji ambao wakiwa uwanjani wamekuwa wakionyesha ubabe kiasi kwamba mpaka sasa unaweza kuwa na kikosi chako cha kwanza chenye wababe tu kama ifuatavyo:-

1. Benedict Tinocco

 Mlinda mlango wa Mtibwa Sugar alionekana akimpiga teke la kichwa mshambuliaji wa Biashara United, Innocent Edwin kwenye mchezo uliochezwa Uwanja wa Nyamagana.
Mchezo huo Biashara United ilishinda mabao 2-1 huku tukio hilo mwamuzi wa mchezo kushindwa kuliona na baadaye Tinnoco aliomba radhi kupitia mitandao ya kijamii.

2. Erasto Nyoni

Beki kiraka wa Simba kwenye mchezo wao dhidi ya Ndanda FC uliochezwa Uwanja wa Nangwanda Sijaona na matokeo kuwa suluhu alimpiga kiwiko mchezaji wa Ndanda, Hassan Nassoro.

Nyoni alipelekwa kamati ya nidhamu ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) na alilimwa faini ya milioni moja na kufungiwa michezo mitatu ya ligi.

3.James Kotei 

Kiungo mkabaji wa Simba alikumbana na rungu la kamati ya masaa 72 baada ya kumpiga ngumi mchezaji wa Yanga,  Gadiel Michael na mwamuzi hakuliona hili tukio ilikuwa kwenye mchezo wa watani wa jadi mzunguko wa kwanza uwanja wa Taifa.

Mechi hiyo ilimalizika kwa suluhu, Kotei alifungiwa mechi tatu na kupigwa faini ya milioni moja baada ya mechi hiyo iliyopigwa September 30 Uwanja wa Taifa.

4.Laurian Mpalile
Nahodha wa Tanzania Prisons, Laurian Mpalile naye pia alionyeshwa kadi ya nyekundu baada ya kuonyesha vitendo visivyo vya kinidhamu kwenye mchezo wao dhidi ya Yanga kwa kumfuata Ngasa ili alipe kisasi cha kumpiga kichwa mchezaji wa timu yake.

Alifungiwa mechi tatu kutokana na adhabu hiyo pia timu yake ilipoteza kwa kufungwa mabao 3-1 ikiwa uwanja wa Sokoine Mbeya.

5.Andrew Vincent

Beki huyu aliitwa kamati ya masaa 72 ya TFF baada ya kucheza mchezo usio wa kiungwana kwa Mohamed Hussen 'Tshabalala' kwa kumpiga kichwa.

Ilikuwa ni kwenye mchezo dhidi ya Simba uliochezwa September 30 uwanja wa Taifa, alipigwa faini ya milioni moja na kufungiwa mechi tatu.

6. Mrisho Ngassa

Kiungo huyu mshambuliaji alionyesha ubabe kwenye mchezo wao dhidi ya Tanzania Prisons baada ya kumpiga kichwa Hassan Kapalata uwanja wa Sokoine na Yanga ilishinda mabao 3-1.

Ngasa alikosa michezo mitatu ya ligi kutokana na adhabu yake hiyo pamoja na kuonyeshwa kadi nyekundu.

7.Abdalah Shaibu 'Ninja'

Beki huyu anayevalia jezi namba 23 aliyokabidhiwa na Nadri Haroub 'Canavaro' alimpiga kiwiko mchezaji wa Coastal Union Anderw Semchimba  mchezo uliochezwa uwanja wa Mkwakwani na kumalizka kwa sare ya kufungana bao 1-1, aliitwa kamati ya masaa 72.

Yanga walikata rufaa ya kupelekwa mbele siku ya kusikilizwa ambapo walikubaliwa shauri hilo likapelekwa mbele ili kusikikilizwa kwenye kikao chao kijacho.

 8.Ayoub Kitala

 mchezaji huyu alifungiwa mechi tatu na kupigwa faini ya laki tano baada ya kumpiga kiwiko mchezaji wa Mbeya City Uwanja wa Sokoine.

Ruvu Shooting walipoteza mchezo huo kwa kufungwa mabao 4-2 wakiwa ugenini ilikuwa Septemba 19/2018.

9.Issa Abushee

Mshambuliaji wa Coastal Union alionyesha ubabe wake mbele ya Gadiel Michael wa Yanga kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa Uwanja wa Mkwakwani.

Abushehe alimchezea rafu Gadiel kulipa kisasi baada ya kuchezewa faulo na mwamuzi kupeta hali iliyofanya aonyeshwa kadi nyekundu kwenye mchezo huo ambao ulikamilika kwa sare ya kufungana bao 1-1.

10.John Bocco

Nahodha wa Simba alikutana na rungu kwenye mchezo wao dhidi ya Mwadui uwanja wa Kambarage ambapo alimpiga kiwiko mchezaji wa Mwadui Revocatus Richard hali iliyopelekea mwamuzi kumuonyesha kadi nyekundu.

Bocco alifungiwa mechi tatu na kupigwa faini ya laki tano wakati Simba ikishinda kwa mabao 3-1.

11.Ahmed Shiboli
Mshambuliaji huyu  wa JKT Tanzania ni pande la jitu linajiamini likiwa uwanjani, alionyeshwa kadi nyekundu na mwamzuzi Mbaraka Ramadhani kwenye mchezo wao dhidi ya Simba.

Licha ya JKT Tanzania kufungwa mabao 2-0 Uwanja wa Mkwakwani, Shiboli alimpiga kibao mwamuzi kwa kulaumu maamuzi yake uwanjani kuwa si sahihi.

4 COMMENTS:

  1. HUYU NI TATIZO. ILI UWE FAIR ITABIDI NAWE UWE REFARII WA PEMBENI KUCHUNGUZI NZ KUWEZA KURIPOTI MATUKIO HSYO YOTE KWA KILA MCHEZO VINGINEVYO UMEWACHAGUA WACHEZAJI USIOWAPENDA UWAANDIKE VIBAYA

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic