March 2, 2019


MCHEZO wa Ligi Kuu Bara kati ya Alliance FC na Yanga umekamilika Uwanja wa CCM Kirumba huku Yanga ya Zahera wakibeba pointi zote tatu.


Kipindi cha kwanza timu zote zilikwenda vyumba vya kumpumzikia bila kufungana, huku Alliance wakimaliza kipindi cha kwanza kwa kutumia nguvu nyingi na waliotea mara moja huku wapinzani wao Yanga wakishindwa kuotea.

Kipindi cha pili Zahera alifanya mabadiliko kwa kumtoa dakika ya 61 kwa kumtoa Boban na Ngasa nafasi na waliingia Tambwe na Banka.

Dakika ya 63 Bigirimana Blaise wa Alliance aliandika bao la kwanza ambalo lilikataliwa kwa mwamuzi kutafsiri ilikuwa ni bao la kuotea.
Dakika ya 75 Amiss Tambwe aliandika bao la kwanza kwa Yanga akimalizia pasi ya Makambo ambaye alikosa penalti dakika ya sita kipindi cha kwanza.

Bao hilo lilidumu mpaka dakika 90 na kuifanya Yanga kubeba pointi tatu leo na kufikisha jumla ya pointi 63 kileleni.



4 COMMENTS:

  1. mbona mnatuficha mwenendo kulikoni

    ReplyDelete
  2. Waamzi Waache Ushabiki Na Wa Epuke Mchezo Wa Kubeti Maana Kwann Aibebe Yanga Amewapa Penati Ya Kizushi Kawanyima Ailiance Penati Na Goli

    ReplyDelete
  3. Miaka ya karibuni sijaona timu ikibebwa kama leo.Hamna haya ya kuwa ns ligi mshindi angetangazwa kwrnyekila mechi kabla.

    ReplyDelete
  4. Mwenye blog anaona aibu kutuwekea matukio kwani ni kashfa.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic