March 3, 2019



FULL TIME: Stand United 0-2 Simba.
Uwanja:CCM Kambarage
Mfungaji mabao mawili ni John Bocco dakika ya 52p,66. 



Dakika 90 zinakamilika Uwanja wa Kambarage,zinaongezwa dakika tatu.

Majaliwa  Shaaban wa Stand United anaonyeshwa kadi ya njano dakika ya 86 kwa kumchezea rafu Niyonzima.

Simba wanafanya mabadiliko ya pili ya lazima baada ya Diliunga kuumia anaingia Mzamiru dakika ya 82.

Stand United wamecheza faulo 11 huku wapinzania wao Simba wakiwa wamecheza faulo 13.

Dakika ya 66 John Boco anafunga goooooli la pili baada ya Niyonzima kupiga kona iliyookolewa na mabeki wa Stand United kabla ya kukutana na Gyan aliyetoa pasi kwa Bocco.

Dakika ya 58 Rashid Juma anatoka anaingia Jonas Mkude.

Dakika ya 52 John Bocco Gooooooo anafunga bao kwa mkwaju wa penalti akitumia guu lake la kulia.

Dakika ya 50 Simba wanapata penalti baada ya Meddie Kagere kupiga shuti lililokamatwa na mchezaji wa Stand eneo la hatari.

Dakika ya 45 Kagere anaotea.

Kipindi cha pili kinaanza Uwanja wa Kambarage mkoani Shnyanga.

Mpira kwa sasa ni mapumziko, nguvu ni sawa hakuna timu iliyoona lango la mwenzake.

Dakika ya 45+4 Datius Peter wa Stand United anaonyeshwa kadi ya njano kwa kumchezea rafu Gyan.

Dakika 45+2 Kagere anaingia akichukua nafasi ya Salamba.

Dakika 45 za mwanzo zimekamilika, zinaongezwa dakika 4 kukamilisha kipindi cha kwanza.

Dakika ya 39 mshambuliaji wa Simba Rashid Juma alidondka ndani ya 18 baada ya kuguswa kidogo na mchezaji wa Stand United karibu na mwamuzi ambaye aliamua  mpira uendelee.

Mpaka sasa  dakika 30 za kipindi cha kwanza zimekatika, Stand United wameotea mara moja huku Simba ikiwa bado hawajaotea.

Mpaka sasa tayari ni dakika 22 zimekatika, Simba wamefanya mashambulizi ya matatu makali huku Stand wakiwa wamefanya mashambulizi mawili, bado milango ni migumu.

Mchezo wa Ligi Kuu Bara kati ya Simba na Stand United unaendelea Uwanja wa Kambarage ikiwa ni kipindi cha kwanza.

Mashabiki waliojitekeza leo ni wengi kuona namna ushindani ulivyo wa wababe hawa wa ligi dhidi ya Chama la wana.

Mpaka sasa hakuna timu iliyoona lango la mpinzani wake huku kikosi cha Stand United kikiwa imara kushambulia lango la Aishi Manula.

Asante Kwasi wa Simba alionyeshwa kadi ya njano dakika ya 11 baada ya kumvuta jezi mchezaji wa Stand United.

Stand United wamepiga kona tano mpaka sasa na Simba wamepiga kona nne ambazo hazikuzaa matunda ila ya tano ilizaa matunda..

4 COMMENTS:

  1. jee akina Kagere na mkude wangeingia tokea mwanzo nini ingelikuwa hatima ya STAND? Oh tutawafunga tutachukuwa pointi tatu. Huyo bwana ni Simba sio yanga. Mnapokabiliwa na mntama chagueni la kusema

    ReplyDelete
  2. Kila mtu ashinde mechi zake. Ikiwa na viporo 6 , Simba inalingana mabao ya kufunga na Yanga,.!bado point 13tu

    ReplyDelete
  3. Zahera anayesifiwa kocha bora kasema ameipa Stand United maelekezo ya kuishinda Simba, lakini wapi bwana. Bora angenyamaza kimya

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic