March 3, 2019





Na Mwandishi Wetu, Antalya 
Wakati kesho ndio kazi inaanza, kikosi cha timu ya taifa ya vijana chini ya miaka 17, Serengeti Boys kitaivaa Guinea, leo kimefanya mazoezi yake ya mwisho kabla ya michuano hiyo.


Kikosi hicho kimefanya mazoezi yake kwenye Uwanja wa Antalya Youth, tayari kwa mechi hiyo ya michuano ya Uefa Assist hapa mjini Antalaya.


 Serengeti Boys inayonolewa na Oscar Milambo kimeonekana kuwa tayari ya hali ya baridi, tofauti baridi na amesisitiza wako tayari kwa ajili ya kazi hiyo ya kesho.



“Baridi ipo lakini si kwa kiwango cha kutufanya kufanya mambo yetu, hatuwezi kuifanya kama kisingizio na tupo tayari kupambana,” alisema.


Mechi hiyo itapigwa kesho saa 5:30 asubuhi kwa muda wa hapa Antalya ambao ni sawa kabisa na nyumbani Tanzania.

Katika kundi la kwanza ambalo Serengeti Boys wapo pamoja na vikosi vya Australia, Guinea na wenyeji Uturuki.



Michuano ya Uefa Assist inafanya kwa mara ya pili na imekuwa ikifanywa kwa pamoja na Shirikisho la Soka Ulaya (Uefa) na lile la Afrika (Caf) katika programu maalum kukuza vijana.

Michuano hii haina bingwa, badala yake ni sehemu ya kujima na kujiendeleza kwa timu za vijana na vijana wenyewe.


Kila timu baada ya mechi tatu za kundi, itaondoka kurejea kwao na kuwaacha wenyeji Uturuki wakiwa nyumbani. Maana yake hakuna bingwa wala kombe.


Serengeti Boys ipo hapa kujiandaa na michuano ya Afcon ambayo itafanyika mwezi ujao nyumbani Tanzania ikiwa mwenyeji.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic