March 3, 2019


LIGI Kuu Tanzania Bara leo imeendelea ambapo timu 10 zilishuka Uwanjani leo na baada ya dakika 90 kukamilika jumla ya mabao tisa yakifungwa katika michezo iliyochezwa leo.

Stand United wakiwa nyumbani walikubali kupoteza mbele ya Simba kwa kufungwa mabao 2-0 mchezo uliochezwa Uwanja wa CCM Kambarage.

Mtibwa Sugar wao wameendelea ubabe wao kwa kuwanyoosha Mbao FC kwa ushindi wa mabao 2-0 mchezo uliochezwa Uwanja wa Manungu.

Kagera Sugar wameitungua Lipuli ya Matola mabao 2-0 mchezo uliochezwa Uwanja wa Kaitaba, Kagera.

Singida United ikiwa chini ya Fred Minziro imepeta leo mbele ya Tanzania Prisons kwa ushindi wa mabao 2-1.

Sare pekee leo imepatikana kwa mchezo mmoja mkoani Mbeya Uwanja wa Sokoine ambapo Mbeya City wamekubali kugawana pointi moja na Ndanda ya Mtwara baada ya dakika 90 kukamilika kwa suluhu ya 0-0.




0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic