March 2, 2019


MABINGWA wa kihistoria Yanga, wameonesha kwamba hawataki mchezo hesabu zao ni kubeba kombe msimu huu ambalo wanadai wamewaazimisha wae wapinzani wao ambao wamebeba msimu uliopita.

Kwenye mchezo wa leo dhidi ya Alliance iliwabidi wasubiri dakika 75 kuwatungua Alliance ambao walikuwa na kasi ya kushambuia ila waliponzwa na uzoefu kwani hawakutumia nafasi ambazo wamezitengeneza wakiwa nyumbani.

Kocha wa Yanga, Mwinyi Zahera amesema wachezaji wake wamefuata maelekezo licha ya kushinda bao moja hesabu kubwa ilikuwa ni pointi tatu muhimu.

"Nilitambua ugumu wa mchezo, niliwaanda wachezaji kisaikolojia hali ambayo imewafanya wawe na morali ya kushinda, kuna ugumu kwenye ligi ila muhimu pointi tatu," amesema Zahera.

Ushinid huo unaifanya Yanga izidi kukaa kwenye ufalme wa kuongoza ligi ikiwa na pointi 64 kibindoni kwa sasa.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic