March 18, 2019


KOCHA Msaidizi wa Lipuli, Selemani Matola, amesema kuwa alitumia CD za Yanga kuwasoma mbinu zao pamoja na uzoefu alionao kwenye ligi kuwamaliza Uwanja wa Samora.

Lipuli juzi ilifanikiwa kulipa kisasi cha bao 1-0 lililofungwa na Heritier Makambo Uwanja wa Taifa kwenye mchezo wa ligi baada ya nao kufunga bao 1-0 kupitia kwa Haruna Shamte.

Akizungumza na Championi Jumatatu, Matola alisema kuwa alitambua ujanja wa Yanga na sehemu ambayo wanaanzia mashambulizi ni kupitia kwa mawinga na mfungaji wao wanayemtegema ni Makambo hali iliyomfanya agawe majukumu.

“Yanga ni timu bora sasa ili kuwafunga wagumu ilibidi nitumie hesabu kali kwa wachezaji wangu, niliwaambia kwamba wasicheze faulo nyingi na Makambo nikampa yule beki wangu mrefu na mwenye nguvu Novarty Lufunga, huyu alikuwa anatembea naye mwanzo mwisho.

“Wachezaji walijituma na walitambua wapo nyumbani hivyo kama ambavyo wao walitufunga kwao basi nasi tumewafunga kwetu, hivyo kwa sasa tunahamishia nguvu zetu mchezo wetu wa Kombe la Shirikisho la Azam Sports dhidi ya Singida United,” alisema Matola.

Lipuli ipo nafasi ya nne kwenye msimamo ikiwa na pointi 44 baada ya kucheza michezo 31 huku Yanga wakiendelea kubaki kileleni wakiwa na pointi 67 baada ya kucheza michezo 28.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic