March 4, 2019


BAADA ya kupoteza mechi zake tatu mfululizo, kocha wa Lipuli ameshangaa mwenendo wa Ligi Kuu Bara kwa sasa kuanza kupoteza dira yake ya awali iliyoanza na namna anavyopata matokeo ya ajabu Uwanjani.

Lipuli ilianza kupoteza kwa Stand United ikiwa ugenini ikarejea nyumbani Uwanja wa Samora, mnyama akainyoosha tena wakati inatafuta pa kutokea Kagera Sugar ikawabonda mazima.

Akizungumza na Saleh Jembe, Matola amesema anashangaa upepo unavyobadilika kila leo kwenye ligi kwakuwa timu inatumia gharama nyingi kujiaanda na kusafiri ila mwiso wa siku wanaangushwa wakiwa ugenini.

"Kufungwa ni kawaida kwa kuwa ni sehemu ya matokeo ila sasa kilicho nyuma ya mechi za ugenini kinawakatisha moyo wachezaji wangu ukizingatia kwa sasa tunapita kipindi kibaya kiuchumi.

"Kuna mengi yanatokea sana hasa kwa mechi ambazo nimecheza nje ya nyumbani, kiukweli ni maumivu tu hadi nawaonea huruma wachezaji wangu kwa namna wanavyopambana wanashindwa kupata matokeo, bodi ya ligi isifumbie macho mechi zetu hasa za ugenini tunapata taabu sana," amesema Matola.

Lipuli imecheza michezo 29 inashika nafasi ya tano kwenye msimamo ikiwa imejikusanyia point 38.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic