March 4, 2019


KOCHA Mkuu wa Coastal Union, Juma Mgunda amesema kuwa wachezaji wake kwa sasa wanapitia kwenye wakati mgumu kwa kukosa matokeo Uwanjani ila bado anawatafutia mbinu mpya zitakazowarejesha kwenye ubora wao.

Coastal Union wamedondosha pointi sita katika michezo yao ya hivi karibuni kwa kuanza na Mtibwa Sugar pamoja na JKT Tanzania hali iliyowafanya wasiwe ndani ya 10 bora kwa sasa kwenye msimamo.

Coastal Union wanashika nafasi ya 11 baada ya kucheza michezo 28 na wamejikusanyia pointi 34 kwa sasa.

"Siwezi kuwalaumu wachezaji wangu kwa kushindwa kupata matokeo, najua wanamaumivu makali ila ni matokeo, kwa sasa tunatazama michezo yetu inayofuata naamini tutapata matokeo kwani kila kitu kinawezekana," amesema Mgunda.

Mchezo wake unaofuata ni dhidi ya Kagera Sugar utakaopigwa Uwanja wa Kaitaba, Machi 09 mwaka huu.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic