March 4, 2019




Na Mwandishi Wetu
Ashura Rashidi Kanyoma wa Tunduru Vijijni ameibuka mshindi wa Jackpoti Bonasi ya Shilingi Milioni 9, 966, 726 baada ya kufanikiwa kubashiri kwa usahihi mechi 11 kati ya 13.

Akizungumza na Waandishi wa Habari, Ashura alisema alianza kubashiri na michezo hiyo ya kubashiri kupitia SportPesa, mwaka jana kabla ya juzi kushinda Jackpoti Bonasi kwa kushirikiana na mume wake, Bakari Sandali.

Ashura ambaye alisema, yeye hafahamu michezo ya kubashiri, lakini kwa kupitia mume wake Bakari Sandali ambaye wamekuwa wakicheza kama familia kufanikiwa kushinda mamilioni hayo kupitia SportPesa.

Alisema kuwa, baada ya kushinda fedha hizo amepanga kuzitumia yeye na mume wake wamepanga kununua kiwanja na haraka wataanza ujenzi wa nyumba yao huko kwao Tunduru vijijini.

“Mimi ni mama wa nyumbani tu ambaye sijishughulishi na kitu chochote, zaidi nipo nyumbani nalea familia yangu, hivyo baada ya ushindi huu nilioupata kwa kufanikiwa kushinda ubashiri wangu wa SportPesa.

“Tulianza kubashiri mimi na mume wangu, mwaka wa jana kabla ya juzi kushinda mamilioni hayo ambayo tumepanga kuyafanyia katika mambo mbalimbali katika kilimo na biashara ambayo mume wangu anayoifanya.

“Hivyo, niwashauri Watanzania kubashiri kupitia SportPesa ambao mshindi akishinda ubashiri wake haraka anawekewa fedha zake,” alisema Ashura mama mwenye watoto wawili ambao ni Fadhili na Azifali.

Kwa upande wa mume wa mshindi huyo alisema kuwa “Anafurahia ushindi alioupata mke wake ambao umetokana na jitihada zake za kumsaidia jinsi ya kucheza michezo ya kubashiri, hivyo niwashukuru SportPesa baada ya ushindi huu ambao utasaidia familia yetu katika kubadilisha maisha yetu sisi kama familia.

Kwa upande wa SportPesa Mkurugenzi wa Uendeshaji Bwana Luca Neghesti alianza kwa kuipongeza familia hiyo kwa kucheza kwa pamoja na hatimaye kuibuka na ushindi wa kiasi cha shilingi Milioni 9, 966, 726.
“Tunapata faraja sana kuona jinsi huduma zetu zinawafikia watu walioko sehemu mbalimbali nchini na kubadili maisha yao hasa kwenye sekta ya kiuchumi nikimaanisha kuwawezesha kukuza mitaji yao na kujiendeleza kama familia”



0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic