March 4, 2019



KOCHA Mkuu wa Mtibwa Sugar, Zuber Katwila amesema kuwa kwa sasa kikosi chake cha Mtibwa tayari gari limewaka hakuna atakayewazuia kupenya katika ligi na lengo lao ni kuwa ndani ya nne bora kwenye msimamo.

Mtibwa wamejikusanyia pointi sita kwenye michezo yao ya hivi karibuni kwa kuanza mbele ya Coastal Union na jana mbele ya Mbao Uwanja wa Manungu, mkoani Morogoro.

"Hakuna tatizo kubwa ambalo linawaponza wachezaji wangu, timu yangu ni bora na ina uwezo wa kupambana, bado nina matumaini ya kurejea kwenye nne bora ya ligi kuu kwa sasa moto hauzimwi," amesema Katwila.

Mtibwa Sugar wapo nafasi ya nane kwa sasa wikwa wamecheza michezo 26 wana pointi 35.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic