March 4, 2019





Na Mwandishi Wetu, Antalya
Kikosi cha timu ya taifa ya vijana chini ya miaka 17, Serengeti Boys kitaivaa Guinea katika mechi yake ya kwanza ya michuano ya Uefa Assist.

Serengeti Boys jana ilifanya mazoezi yake ya mwisho kabla ya mechi ya leo ambayo ni ya Kundi la Kwanza na timu nyingine zilizo katika kundi hilo ni wenyeji Uturuki pamoja na Australia.

Mechi hiyo itapigwa leo 5:30 asubuhi kwa muda wa hapa Antalya ambao ni sawa kabisa na nyumbani Tanzania.

Kocha Oscar Mirambo amesema wako tayari na suala la changamoto ya maumbo makubwa ya timu nyingine, haimpi hofu.


Mirambo amesema ni sehemu ya mafunzo na kikosi chake kipo tayari kwa ajili ya mechi zote tatu ikianza na hii ya leo.

Serengeti Boys jana ilifanya mazoezi yake huku Mirambo akiandaa mambo kadhaa yakiwemo yale ya ulinzi wa faulo lakini pia upigaji wa krosi.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic