March 3, 2019



KOCHA wa Mtibwa Sugar, Zuber Katwila amesema baada ya kupata ushindi wa kwanza mwaka huu mbele ya Coastal Union kwa ushindi wa mabao 3-1, leo ni zamu ya Mbao FC hakuna mchezo utakaopigwa Uwanja wa Manungu.

Mtibwa Sugar, walitumia dakika 810 bila kupata ushindi zaidi ya kupata sare tatu na kupoteza michezo sita ambayo waliicheza mwaka huu mwezi Januari na Februari.

Ilianza mwaka kwa kupoteza mbele ya Prisons (1-0), Mbeya City (1-0), Lipuli (1-0) ikalazimisha suluhu na JKT (0-0) Ndanda (0-0) ikalazimisha sare na Africa lyon  (1-1) kabla ya kupoteza kwa  Biashara United (2-1) Mwadui (1-0) na  KMC (1-0).

"Mwendo wetu sio mbaya na ninatambua ushindani uliopo kwenye ligi kwa sasa, wachezaji wana morali kubwa na wanatambua kazi yao ni kuona wanapata matokeo, hivyo mwendo wetu kwa sasa ni pointi tatu muhimu," amesema Katwila.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic