March 9, 2019

MSHAMBULIAJI wa Simba, Meddie Kagere 'Mzee wa kutetema' amewataka mashabiki waiombee dua Simba kwenye mchezo wao wa leo dhidi ya JS Saoura ya Algeria ili waibuke na ushindi.

Simba watamenyana na JS Saoura leo ikiwa ni mchezo wa marudio wa Ligi ya Mabingwa Afrika wakiwa na kumukumbu ya ushindi wa mabao 3-0 kwenye mchezo wa kwanza uliopigwa Uwanja wa Taifa.

Kagere amesema kuwa ushindani ni mkubwa na kila timu inapiga hesabu kubeba pointi ila imani yao ni kuona wanaibuka washindi kwa kuwapiga wapinzani wao nje ndani.

"Kwa sasa hesabu zetu ni kuona tunapata matokeo kwenye mchezo wetu wa kimataifa.

"Sio jambo jepesi kama ambavyo wengi wanafikiria kutokana na utofauti wa mashindano ulivyo ila bado tuna nafasi ya kufanya vizuri, tutapambana ili kupata matokeo mashabiki wetu waendelee kutuombea," amesema Kagere.

Simba leo wanashuka Uwanjani kuwakabili wapinzani wao JS Saoura majira ya saa 4:00 Usiku Uwanja wa 20 Aout 1995 unaoingiza mashabiki 15,000 uliopo mjini Bechar.

1 COMMENTS:

  1. Tunanyanyua mikono miwili kumuomba Rahmani aliyeumba mbingu na ardhi mwenye kila ya uwezo ampe ushindi mnono Mnyama Inshallah

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic