MSHAMBULIAJI wa timu ya Uganda, Emmanuel Okwi amemaua kuwachunia mazima watanzania ambao wamekuwa wakimuomba asiwakazie siku ya Jumapili Uwanja wa Taifa kwenye mchezo wa kufuzu hatua ya Afcon.
Okwi ambaye akiwa bongo anakipigia kwenye timu ya Simba ni miongoni mwa wachezaji ambao watamenyana na Tanzania siku ya Jumapili katika mchezo wao wa mwisho ambao watanzania hesabu zao ni kuona wanapata matokeo chanya ili kusonga mbele kwenye michuano ya Afcon itakayofanyika mwezi June nchini Misri.
Kwenye Ukurasa wake wa Istagram Okwi alitupia picha akiwa na mchezaji mwenzake wa Uganda, Juuko Murshid ambaye naye anakipiga Simba akisindikiza na maneno "majukumu ya Taifa" hapo ndipo watanzania walipoanza kudondosha maoni yao kumtaka Okwi asiifunge timu ya Tanzania ambayo hayakujibiwa na Okwi.
Miongoni mwa rafiki yake ambaye mara nyingi amekuwa akimjibu, Joseph Owino ambaye alikuwa ni mchezaji wa Simba raia wa Uganda aliandika "Usiwaadhibu kaka zetu tafadhali," na baada ya yeye kuanza ndipo wengine zaidi ya 100 waliendelea kumpiga mkwara Okwi, ndipo Owino alipoona kimya akasema " Nitamfuata kwa ujumbe wa WhatsApp kwa kuwa namba yake ninayo mimi," amesema Owino.
Stars wameshaanza mazoezi kwenye Uwanja wa BocoVeteran kwa ajili ya kujiwinda kuimaliza Uganda ambayo tayari imefuzu hatua ya Afcon kwenye kundi L.
0 COMMENTS:
Post a Comment