March 3, 2019


Kikosi cha timu ya taifa ya Tanzania chini ya umri wa miaka 17 kimetua salama jijini Antalya nchini Uturuki tayari kwa michuano ya UEFA ASSIST ambayo hushirikisha vijana wenye umri chini ya miaka 17.


Serengeti Boys imetua jijini Antalya baada ya safari ndefu angani ikipita katika miji ya Dubai na Istanbul na leo itaanza rasmi mazoezi kujiandaa na michuano hiyo itakayoshirikisha timu nyingine za Afrika ambazo ni Guinea, Uganda na Nigeria.

Mashindano hayo yanayoshirikisha timu 12 kutoka duniani kote, yatakuwa ni sehemu ya maandalizi kwa Serengeti Boys kuelekea michuano ya AFCON kwa vijana chini ya umri wa miaka 17 yatakayofanyika jijini Dar es Salaam mwezi Aprili mwaka huu.

Serengeti Boys ipo kundi 1 na timu kutoka
1. Uturuki 
2. Guinea na
3. Australia

Kila la kheri Serengeti Boys!

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic