March 3, 2019



BAO la Amiss Tambwe jana dhidi ya Alliance dakika ya 75 akimalizia pande la pasi ya Heritier Makambo limeongeza mzingo kwa mabingwa watetezi Simba kuifikia kwa sasa.

Pointi tatu walizobeba jana zinaifanya ifikishe pointi 64 kwenye msimamo wake ikiwa ni namba moja huku Simba wakiwa na pointi zao 48 baada ya kucheza michezo 19 kwenye ligi msimu huu.

Kwa ushindi huo Yanga wamewaongezea mzigo wa pointi 16 ili wawafikie hapo walipo na kama watakuwa na presha kazi itazidi kuwa ngumu kwani watakuwa wanakula viporo wakiwa na presha pamoja na mzigo huo wa pointi 16.

Kocha Mbelgiji Patrick Aussem, kawatazama wachezaji wake kisha akawaambia mashabiki wasiwe na hofu kazi nyepesi kwake kwani hesabu zake ni kubeba pointi tatu muhimu.

"Ipo wazi tuna ratiba ngumu na ushindani ni mkubwa, uwezo wa wachezaji wangu unaimarika kila siku na malengo yangu ni kushinda kila mechi, sina hofu, hivyo mashabiki wasiwe na presha kila kitu kinawezekana," amesema Ausem.

Sima leo watashuka kumenyana na Stand United wakiwa na kumbukumbu ya kushinda mchezo wao wa kwanza walipokutana Uwanja wa Taifa kwa mabao 3-0.

1 COMMENTS:

  1. Mungu ni mkubwa na muweza, Mnyama ataingia kufuwa mbele na kutoka nyuso juu, atacheka ataecheka na kulia ataelia wembe ni uleule wa mwanzo, lakini umezidi kunolewa

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic