Akizungumza kupitia radio Uhuru, Mwakyembe ameeleza kuwa Yanga inapaswa kufanya uchaguzi huo baada ya kuona hakuna mipango yoyote inayoendelea.
Ameeleza kuwa kuna kikao kizito hivi sasa kinaendelea baina ya Yanga, TFF na Serikali kuhakikisha uchaguzi huo unafanyika.
Ikumbukwe Yanga ilipaswa kufanya uchaguzi huo mwanzoni mwa mwezi Januari mwaka huu lakini ulisimama baada ya wanachama baadhi wa klabu hiyo kufungua kesi mahakamani.
0 COMMENTS:
Post a Comment